Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad
Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa
Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.
Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa
Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL
walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.
Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema
(BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji
wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza
Watutsi.
“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua
hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa
amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda,
amempandisha cheo,” alisema.
Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.
Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na
Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa
Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.
Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia
mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na
dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.
CHANZO: NIPASHE
Home
»
»Unlabelled
»
DR. SLAA AMVAA RAIS KIKWETE KUHUSU MGOGOLO WAKE NA KAGAME
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment