TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

ASKOFU wa kanisa la full gospel bible fellowship amekanusha uvumi ulio tapakaa kwa Watanzania yakuwa amewakimbia wakristo wake na kuenda nchi za nje.
Alikanusha uvumi huo baada ya kuongoza mazishi ya aliye kuwa Askofu wa kanisa la Christian Love lililopo  Kiwalani, aliyefaliki tarehe 2 Agost mwaka huu.
Mazishi ya mcungaji huyo yaliambatana na ibaada ambayo iliongozwa na Kakobe katika makaburi ya Kinondoni juzi.
kakobe aliongea na mwandishi wetu na kumwambia kuwa yeye hajaondoka nchini kama Watanzania wengi wanavyo sema.
"sijaondoka na siwezi kuondoka kwasababu mimi ni wa hapahapa na nitazidi kuwa hapahapa, na tutabanana hapahapa hakuna kwingine tena. Huwa natoka kihuduma tu na huwa narudi tena, na sio kuwa nimehama", alisema Kakobe
kumekuwa na ukimya saana kwa Askofu huyo kitu kinacho washangaza wengi, kwani walisha zoea kumuona akiongea kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.
mmoja wa wakristo wake alikili kuwa kwa sasa Askofu wao amepoteza umaarufu tofauti na zamani ndio maana watu wengi wanafikia uamuzi wa kufikiri hayupo nchini.
Kwaupande mwingine kinacho shangaza ni kwamba ujio wake katika msiba huo wa Askofu mwenzake ilikuwa ni safari ya kutokea nchi za nje ambapo aliingia nchini siku ya jumapili ya Agost mwaka huu.

0 comments :

 
Top