A: Saada Mkuya awa waziri wa fedha manaibu ni Mwigulu Nchemba na Adam Malima....
B: Wizara ya Sheria na Katiba amepewa Dr Asha-Rose Migiro na naibu wake ni yule yule Angela Kairuki
C: Wizara ya Elimu waziri ni Shukuru Kawambwa na naibu ni Jenister Mhagama. Philip Mulugo ameondolewa kabisa serikalini
D: Wizara ya Mifugo na maendeleo ya uvuvi waziri ni Dr Titus Kamani, Naibu wake ni Kaika Telele. Ole Nangolo ameondolewa serikalini.
E: Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto, Waziri ni Sophia Simba, naibu wake ni Pindi Chana, Umy Mwalimu amehamishiwa Muungano.
F: Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi waziri ni Anna Tibaijuka, Naibu ni George Simbachawene
G: Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika waziri ni yuleyule Christopher Chiza na naibu ni Godfrey Zambi. Adam Malima amehamishiwa wizara ya Fedha
H: Wizara ya Nishati na Madini, waziri ni yuleyule Prof Muhongo, manaibu ni Steven Maselle na Charles Kitwanga. Simbachawene yuko Ardhi
I: Wizara ya Maliasili na Utalii waziri ni Lazaro Nyalandu na naibu wake ni Mahamoud Mgimwa mbunge wa Mufindi Kaskazini
J: Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Waziri ni yuleyule Dr. Fenella Mukangara, naibu ni Juma Nkamia mbunge wa Kondoa Kusini.
K: Wizara ya Mambo ya ndani waziri ni Mathias Chikawe aliyekuwa sheria na katiba, na naibu wake ni yuleyule Pereira Sillima.
L: Wizara ya Afya aliyekuwa naibu Dr. Seif Rashid amekuwa waziri na naibu wake ni Mbunge wa Serengeti Kebwe Stephen Kebwe.
M: Wizara ya Ulinzi na JKT Waziri ni Dr Hussein Mwinyi aliyekuwa Waziri wa Afya
N: Wizara za Uchukuzi, Ujenzi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya waziri Mkuu Mambo ya nje, Afrika Mashariki, Mawasiliano, Kazi. Hakuna mabadiliko
Wizara ambazo hazina mabadiliko ni: Wizara za Uchukuzi, Ujenzi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya waziri Mkuu ,Mambo ya nje, Afrika Mashariki, Mawasiliano na wizara ya Kazi.
Sura mpya katika baraza lililotangazwa ni:- Mwigulu Nchemba, Stephen Kebwe, Pindi Chana, Zambi, Juma Nkamia, Kaika Telele, Jenister Mhagama, Mahmoud Mgimwa na Dr. MigiroSee More
Moja kati ya mawaziri ambao walitajwa kuwa mizigo katika wizara zao ni waziri wa elimu bwana Shukuru Kawambwa ambae anaendelea na majukumu yake katika wizara hiyo.
0 comments :
Post a Comment