TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Soko la Kariakoo
Wafanyabiashara katika viunga vya Kariakoo, Wilaya ya Ilala wamegoma kufungua maduka leo ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Sababu za mgomo huo ni kupinga amri ya Seriakali kuhusu matumizi ya mashine za kielectronic (EFD). Migomo ya namna hiyo imeripotiwa katika miji ya Musoma, Mwanza, Iringa, Mbeya nk. Migomo ya namna hii inahatarisha uchumi wa nchi ambao uko katika kipindi kigumu kuliko muda wowote katika mwongo huu.

Je, si wakati muafaka kwa Serikali kukaa chini na kutafakari maamuzi yake?

Kariakoo ni eneo ambalo ni muhimu sana katika kuingizia serikali mapato pengine kuliko eneo lolote nchini. Zaidi ya hayo ni eneo ambalo hutegemei mfanyabiashara atengeneze faida kubwa kulingana na makato yanayotakiwa kufanywa kwa kila mauzo...

Tujadili mada hii kwa hoja za msingi ili kunusuru uchumi wetu!

Source Jamiiforum

0 comments :

 
Top