Chuo Kikuu cha Bolton nchini Uingereza leo kimemtunukia udaktari wa heshima Ryan Giggs
kutokana na mchango wake uliotukuka katika michezo.
Tukio hilo lilifanyika Katika sherehe iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Victoria chuoni hapo.
Makamu mkuu wa chuo Profesa George Holmes amesema Dr. Ryan Giggs ametukuka katika maisha yake, huku mchango wake ukitia fora.
Pia, Dr, Ryan Giggs alipata wasaa wa kuhutubia halaiki ya wasomi waliohudhuria tukio hilo.
Mwaka 2007 Malkia wa Uingereza, Elizabeth Wa Pili
alimtunuku Ryan Giggs nishani ya juu ya OBE. Mwaka uliofuatia alitunukiwa MA kutoka Chuo
Kikuu cha Salford cha nchini humo.
Dr. Ryan Giggs ambaye ameichezea Manchester United kwa misimu 23, sasa ni kocha msaidizi wa Louis van Gaal.
By Yunge Kanude.
0 comments :
Post a Comment