TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mtazamo wangu juu ya nani anaeweza kuwa rais wa nchi hii. Pamoja na mapungufu mengi aliyonayo Lowasa bado anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuwa Rais wa Tanzania kutokana na mambo yafuatayo:

Mosi, Lowasa amefanya maandalizi ya kutosha. Mtakumpuka safari ya huyu jamaa imeanza punde tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2010. Ametembea kila mahali, makanisani, misikitini, Concerts mbalimbali nk. Uzoefu unaonesha maandalizi mazuri huleta matokeo mazuri.

Pili, Pamoja na kuandamwa na kashifa ya ufisadi, Wapinzani wake bado wanaonekana kuwa wepesi kwake. Mfano, mtu kama Mama Migro bado kwa nature ya nchi zetu za kiafrika hatujajiridhisha kama kina mama wanauwezo mkubwa kiasi hicho na pia na actual partial capability aliyoionesha alivokuwa naibu katibu mkuu wa UN.

Membe pia ameshindwa kijitofautisha na JK completely. Watanzania wanahitaji rais wa tofauti kidogo.
Pamoja na kuonesha utulivu pamoja na kujituma katika nafasi yake ya ubunge wa Bumbuli, Makamba bado anaonekana kuwa mbichi hivyo makada wa chama chake akiwemo mwenyekiti wamemtaka kuvuta subira.
Wengine wengi kama Kinana, Sitta, Wasira, Mwakyembe , Ngeleja, Kingwangala n.k bado wanaonekana kutokuwa na social capital ukilinganisha aliyonayo Lowasa.

Tatu, Lowasa anaonekana kuwa na nafasi ya kuachiwa usukani kuendesha jahazi hata nje ya CCM.
Nne, Ni swala lisilopingika kuwa uwezo wa kifedha katika nyanja hii haliepukiki. Katika hili Lowasa bado amewashinda wenzake.

Tano,Chama chake kina hofu na Lowasa. Hofu hii inatokana na kumeguka ikiwa mbwana mkubwa ataamua kuhamia upande wa pili wa shilingi na hofu inayotokana na kuanikwa hadharani ikiwa watamtema.
Mwisho, Lowasa nafasi yake ya kuwa rais inaweza kupukutika ikiwa vyama vya upinzani vitafanya kazi ya kutosha kuwa na umoja stahimilifu pamoja na kufanya kazi ya kujijenga vyema kisiasa na kutoruhusu migawanyiko pamoja ubinafsi. Kibubu cha kisiasa kwa upande huu bado kinayo nafasi kubwa inayohitaji kujazwa kama Kuna lengo la kupata ushindi.

N.B...kumpokea Lowasa(Opposition) endapo atakwamishwa ndani ya CCM pia kunaweza kukasaidia kwa kiwango kikubwa kufanikisha Mabadiliko ya kisiasa nchini.

Chanzo. Bob Chacha Wangwe

0 comments :

 
Top