TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es salaam
Ndugu Watanzania, kumekuwa na kasumba kwa viongozi wa Afrika kuwa na ubabe ambao ni wa kuwaonea wananchi wao wenyewe na hata kwenda tofauti na katiba za nchi, kikundi au chama chochote kile. Kasumba hii imekuwa ikijitokeza hata katika ngazi ambazo ni za kujifunzia uongozi hasa mashuleni na vyuo vikuu.

Ubabe huu umejitokeza kwa Rais wa Serikali ya wanafunzi, Chuo kikuu cha Dar es salaam(DARUSO), Nikson Filbert, ambapo amekuwa akifanya mambo mengi ambayo yanakuwa nje ya maamuzi ya wabunge au katiba ya DARUSO inavyosema.

Rais huyo tangu aanze kuiongoza serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam mnamo mwezi wa tano mwaka huu amekuwa akifanya maamuzi ambayo si sahihi na hayaendani na matakwa ya Bunge rasimi la serikali ya wanafunzi. amekuwa akibadilisha mambo mengi ambayo anaona kwa mtazamo wake yeye yatampandisha hadhi na kuwa kiongozi bora.

Alipoingia madarakani tu, akaja na sera ya kupunguza idadi ya mawaziri na idadi ya kamati za kudumu, jambo ambalo ni zuri na ni jema katika serikali yake na kwa kupunguza matumizi ya serikali ya Wanafunzi kwa ujumla.

Jambo ambalo alianza kuonyesha ubabe ni katika uteuzi wa Mawaziri wa Seriksli ya DARUSO, kwani hakufuatiia zaidi juu ya ushauri wa toka pande mbalimbali, kuwa nani anafaa kuwa Waziri wa wizara mbalimbali za DARUSO. Mawaziri wengi aliowachagua hawana ushawishi katika mambo mbalimbali, pia sio makini katika utendaji wao. Kwa mfano Waziri wa fedha ni waziri ambaye alishindwa kuandaa bajeti ya serikali ya wanafunzi DARUSO kwa mwaka 2014/2015 hali iliyopelekea Bunge kutopitisha bajeti hiyo.

Ubabe wa pilii ni pale ambapo alianza kulazimisha bajeti iliyo katataliwa na Bunge la Serikali ya Wanafunzi. Sababu ya kuipinga bajeti hiyo ilikuwa ni kutoweka baadhi ya mapato ya DARUSO, kama vile, mapato ya magari yanayotumika kusafirisha Wanafunzi, posho ya mawasiliano kwa wabunge shilingi 250 kwa siku, idadi ya viongozi wanaotakiwa kubaki kwa ajili ya kushughulikia Wanafunzi wanaokuwa katika mafunzo ya vitendo(field)

Utata juu ya yote hayo ulikuwa juu ya pesa zitakazotumika kulipa poshoo hizo kwani inavyoonekana Nickson analengo la kubana matumizi ili aache kiasi kikubwa cha pesa atakapomaliza uongozi wake ili aje kuzawadiwa uongozi bora  kama alivyofanyiwa alipokuwa mwenyekiti wa kitivyo cha sheria 2013/2014.

Kwa mvutano mrefu zaidi, Nickison akiwa anagoma bajeti kurudi tena bungeni na hivyo kutaka kuipitisha kama yeye anvyotaka na bila Bunge kuzingatiwa juu ya mapendekezo yake katika marekebisho ya bajeti hiyo. Hatimaye alikubalik urudisha bungeni mjadala wa bajeti na hivyo kukubali mapendekezo ya Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, bado msimamo wa Nickson ukawa ni uleule kwa upande wa idadi ya Viongozi watakaobaki chuoni, na hivyo kusisitiza kuwa atabaki kiongozi mmoja tu kila kitivo. jambo ambalo limekuwa likipingwa na wabunge pamoja na wenyeviti wa vitivo vyoote vya Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Jambo hili limesababisha usumbufu kwa viongozi hao kwani wengi walijua watabaki mazingira ya chuoni na kusababisha kutafuta field maeneo jirani na chuo, kwa namna yoyote ile hata kama sio sehemu wanazofurahia kufanyia mafunzo kwa vitendo. lakini uamzi wa raisi wa kubaki kiongozi mmoja, umewafanya kuhaha sehemu zingine za kufanyia mafunzo kwa vitendo.

Viongozi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ubabe huo, wa kutozingatia maamuzi ya Bunge ambayo yaliafikiwa katika kikao cha mwisho cha kupitisha bajeti ya 2014/2015

Mpaka sasa mgogoro unaendelea na kufanya mambo yawe magumu zaidi kwa viongozi kuthaminiwa na Wanafunzi waliowachagua hasa wanapopata matatizo ya field. Kwani hadi sasa baadhi ya vitivo wanafunzi hawajapata sehemu za kufanyia field na kiongozi mmoja hawezi kushughulikia idadi kubwa ya wanafunzi wenyematatizo na field.

Wengi wao wamekuwa wakisema msimamo wake wa kutaka kubana bajeti ya pesa za kubaki, si kigezo cha kufanya awe kiongozi bora. kiongozi bora ni yule anayefanya mambo kulingana na makubaliuano na viongozi wengine anaosaidiana nao katika uongozi wake. Na watashangaa saana kama kweli atapewa hiyo sifa ya kuwa kiongozi bora kwa kutunza kiasi kukubwa cha fedha ikiwa anaenda tofauti na mapitisho ya Bunge.

0 comments :

 
Top