TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

The service to Widows Ophans ans the Little one Organisation (SWOLO) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiliwa na inatambulika kisheria iliyoko wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya, inayojishughulisha na masuala ya kijamii hasa kusaidia wanawake wajane wazee kuanzia miaka 60 na kuendelea, watoto yatima ammbao walezi waohawana uwezo, watoto wadogo (wtukutu).
Asisi hii inaongozwa na Murugenzi Abel Ambakisye, ambaye amekuwa akifanya kazi ya kuhamasisha na kutoa ushauri kuhusu haki za  wazee. Lakini pia asasi inamlezi ambaye ni mwanasheria Mhe. Jaji mstaafu Raymund Mwaikasu ambaye amekuwa mshauri mkubwa saana kwa asasi hii.
Asasi hii ilianza kufanya kazi mnamo tarehe 15/06/1995 kwa kulitangazia taifa tatizo la watoto yatima kwa uzito mno kupitia redio tanzania dar es salaam kwa wakati huo, ITV, na katika vyombo vya habari vingine kama vile magazeti. Hii ilfanya jamii kuamuka na kuunda ASASI zilizo jitokeza kusaidia watoto yatima na baadhi ndio hizi zinazoendeshwa mpaka sasa.
ASASI hii ilishindwa kufikia malengo yake ya kuwaweka pamoja watoto yatima na kujenga zahanati za kuwahudumia walengwa kutokana na kukosa misaada ya kutosha kutoka kwa jamii na kujikuta ikiwa katika upande  wa utetezi na, ushawishi na ushauri kwa walengwa.
SWOLO ilikuwa chachu kwa jamiii kujua zaidi umhimu wa ASASI na kufungua ASASI nyingi nchini ambazo zilikusudia kusaidia watoto yatima na watoto wa mitaani.
MAFANIKIO YA ASASI
Mnamo mwaka 2000 SWOLO iliteuliwa kimkoa kuziwakilisha  asasi zisizo za kiserikali kushiriki katika warsha iliyokuwa imeundwa  nashirika la kimataifa la Help Age linalotetea haki za wazee kwa ujumla.
Akielezea hatua hiyo Mkurugenzi wa SWOLO, Ambakisye alisema kuwa waliteuliwa kwa sababu ni ilikuwa ni asasi iliyokuwa inautendaji m zuri kwa jamii na ushirikiano mzuri na shirikak hilo la Help Age na mpaka sasa wanaendelea na ushrikiano huo.
Pia mwaka 2003 asasi hii ilishiriki warsha ambayo iliitishwa na shirika la Help Age iliyo shirikisha TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA nchini ikihusu HAKI ZA WAZEE.
Asasi hii ni ya kwanza kuanzisha mafunzo ya awali ya kidato cha kwanza kwa wilaya wa Kyela huku ikianzisha pia darasa la Elimu ya watu wazima likiwahusisha watumishi wengi walioishia darasa la saba..
Mafanikio makubwa hasa ambayo ni ya kujivunia kwa asasi hii na jamii kwa ujumla ni kuunda mabaraza ya wazee katika kila kijiji na kila kata huku kukiwa na viongozi wanaoyaongoza mabaraza hayo kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya kata.
Pia imefanikiwa kutetea na kutoa elimu kuhusu mambo makubwa mawili yaliyomo katika sera ya serikali
·         Matibabu bila malipo kwa wazee wote wenye umri kuanzia 60 na kuendelea tofauti na hapo nyuma ambaposerikali ilidai kuwasamehe wazee wasiojiweza tu.
·         Penseni ya kinga (protection pension) kwa wazee wote ambao ni Watanzania kuanzia miaka 60 na kuendelea bila ya kujali sekta yake ya utumishi kwa umma uma wetu, aidha Mkulima , Mvuvi, Mfugaji, Mtumishi wa Kanisa, Mfanyabiashara N.K

KWA MCHANGO WAKE WOTE HUO ASASI HII INATAKIWA KUKUMBUKWA NA KUPEWA USHIRIKIANO ZAIDI ILI IZIDI KUFANYA KAZI ZAIDI YA KUTETEA WAZEE NA WAJANE.
Kwa mawasiliano na SWOLO
Telephone +255 2540320
Mobile       +255 787413200
                   +255 759371317

Email  swolo1992@yahoo.co.uk

0 comments :

 
Top