"Nikufundishe nini mwanangu kuhusu wanawake?
Baba yako nimezeeka ghafla nikiwa na ufahamu
mdogo na mwanangu umeshakua kiasi cha kuhitaji
elimu hii adhimu, nikupe neno gani?, labda hivi,
1.Kuhusu Tamaa zao. Mwanamke yeyote anaweza
kukutamani kimapenzi isipokuwa Mama yako.
2. Kuhusu hulka zao.Wanawake wote huonesha
upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa
kabla.
3.Kuhusu kuachana.Mwanaume kumuacha
mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha
kula swala, Mwanamke kumuacha mwanaume ni
rahisi kama swala kumkimbia Simba mzee.
4.Kuhusu tabia. Jihadhari na maneno ya vijiweni
kwamba wanawake wote wako sawa kitabia. No,
lakini kumbuka hakuna Mwanamke asie
Mwanamke.
5. Kuhusu mpenzi Wa zamani. Kujaribu kumsahau
mwanamke uliyewahi kumpenda ni kama
kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni ngumu.
6. Kuhusu kuoa. Muhimu kuoa, na ni ngumu sana
Kumjua mke mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji
wazuri sana. Kumbuka maneno ya wewe mwana "
Muhimu kuoa, ukipata mke mwema utakuwa na
furaha, ukipata mke mwovu utakuwa mwanafalsafa.
7. Kuhusu usaliti. Vizuri kujiandaa kisaikolojia
kusalitiwa, la usipojiandaa ama waweza kuua mtu
au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa
furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao
waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya
ulivyokuwa hai.
8.kuhusu pesa na mapenzi. Mapenzi bila pesa
yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni, hapa
duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna
makubaliano bila pesa. Omba mungu.
9. Kuhusu uongo. Wahenga walisema Ukweli
unauma, Na mimi nakuambia "Uongo unaua"
10. Kuhusu kuwajua wanawake. Ewe mwanangu,
kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi ya
kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Usihangaike na
vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba
za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna
kanuni moja tu ya kupenda, " ili ubaki salama
katika kupenda sharti ujipende kwanza".
...Basi mwanangu hayo ndio machache naweza
kukuhusia, na wewe una nafasi ya kujifunza zaidi
na kufundisha kwa ufanisi zaidi kuliko Mimi...
Hekima zangu ziwe kama msingi... zitumie
kujijenga.
0 comments :
Post a Comment