
Mzee Hassan Nassoro MOYO ameeleza jinsi alivyoshiriki kuinusuru znz kuingia kwenye umwagikaji wa DAMU mkubwa baada ya CCM kushindwa kwa mbali ktk uchaguzi wa mwaka 2010.
MOYO asimulia alivyotumwa kumwangukia Maalim Seif akubali ushindi HARAMU wa CCM znz baada ya Rais wa znz Aman Karume na mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete kumwagiza kufanya hivyo.
"Mimi ndiye niliyetumwa na mwenyekiti wa CCM(kikwete) na Rais Karume akafanye kile ambacho anaamini ndiyo kilichoviepusha visiwa hivyo na machafuko baada ya mwenyekiti wa CCM taifa na Rais Karume kusema wako tayari kwa lolote lkn sio kumtangaza mshindi (Maalim self)"
Akisimulia, MOYO ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maridhiano ya watu sita znz alisema "saa chache kabla ya Tume ya uchaguzi znz kutangaza matokeo urais, alikutana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Chama Cha Wananchi Cuf Maalim Seif Sharrif Hamad.
Akisimulia kuhusu mkutano huo, MOYO alisema alikwenda kuonana na kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa znz baada ya kuombwa na aliyekuwa Rais wa znz Aman Karume na mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete.
"Siku ya kutangaza matokeo ya urais 2010 alikuja kijana hapa kwangu USIKU Eddy Riyami majira ya 10:00 aifajiri akasema ametumwa na Rais Aman Karume nikamuone Maalim Self , Nikauliza kunanini, nikazungumze nae nini? "
"Nikamuliza Eddy je tumeshindwa? akatabasamu(smile) akasema NDIYO tumeshindwa.Mimi ni mtu nikasema siondoki mpaka nisali, nikasali mpaka saa 11:30 tukaondoka na gari yake mpaka kule.
MOYO ambaya alikuwammoja wa wazanzibar waliounda Baraza la kwanza la Mapinduzi chini ya Hayati Abedi Karume anamini kwamba ushawishi wake kwa Maalim Seif ndio hatimaye uliosaidi kuvioko visiva vyetu na umwagikaji mkubwa wa DAMU hasa kutokana na msimamo wa CCM kuwa wapo tayari kwa lolote lkn hawawezi kumtangaza mshindi halali(Maalim Seif)
Hatimaye kutangazwa kwa matokeo yaliyompa ushindi Mhe Shein ushindi wa 50.1 dhidi ya 49. uliotangazwa kupata Maalim Seif.
"Tukaonana na Maalim Seif na tulikutana na vijana wengi wamekusanyika. Gari tuliacha msikitini kule, baadhi ya vijana wakaniuliza Moyo unakwenda kupigania serikali yetu? Ndiyo mara ya kwanza naingia kwenye ofisi za Cuf , Mlandege alisema Moyo" Akizungumza hali ilivyokuwa katika ofisi za Cuf alisema aliwakuta baadhi ya makada wa chama hicho akiwemo Juma Duni Haji, Ismail Jussa, Machano Khamis, na Al Haji pamoja na Maalim Seif .
MOYO alisema kwa sababu hakutaka maongezi yake na Seif yasambae aliwaomba wawapishe isipokuwa Jussa na Eddy
. "Nilizungumza na Maalim Seif kwa saa1:30 huku yeye akiwa ananitazama tu bila kusema lolote " mimi sisemi kwa kubahatisha, sio mtu mwa kubabaisha, wala siogopi sikuubwa kuogopamimi." Baada ya kumaliza nikamwambia, aliyonituma ndugu yako Aman Karume kwamba yakitangazwa matokeo Jioni ya leo uyakubari........Endelea kufuatilia sehemu ya pili kesho
0 comments :
Post a Comment