1. UTANGULIZI
Ndugu wana habari, tumewaita hapa ili kuwaeleza Watanzania kupitia kwenu mambo matatu makubwa ambayo ni ;
i. Kuujulisha umma azma ya kuendeleza Ushirikiano wetu kuanzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa mpaka Uchaguzi Mkuu 2015.
ii. Hatima ya Katiba : Katiba ya wananchi haiwezi kupatikana chini ya utawala wa CCM.
iii. Tangazo la Mkutano wa UKAWA tarehe 26/10/2014 na kusaini Makubaliano ( MOU ) ya ushirikiano wetu.

2. JUU YA “KATIBA INAYOPENDEKEZWA”
Ndugu wanahabari, kwa muda sasa kumekuwa na sintofahamu juu ya kile kilichotolewa na kundi la wajumbe wa lililokuwa Bunge Maalum la Katiba na kumkabidhi Rais Kikwete kama ‘Katiba Inayopendekezwa’. Tunataka kuwajulisha kuwa kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011, Katiba inayopendekezwa inapaswa kuwa na sifa kuu tatu:
i. Itokane na Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
ii. Ipitie maboresho kwenye BMK, Ipitishwe ibara kwa ibara kwa kura zisizopungua theluthi mbili kutoka kila upande wa Muungano, yaani Tanganyika na Zanzibar.
iii. Katiba inayopendekezwa ipigiwe kura ya Maoni na wananchi.
Kile kilichokabidhiwa Rais kimeonekana wazi kuwa kimepungukiwa sifa zote hizo: yaani haikutokana na rasimu iliyowasilishwa Bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Na baadala yake kimetokana na rasimu ya giza na maoni yaliyokusanywa na Samuel Sitta na washirika wake, na kuyatupilia mbali maoni ya wananchi kwenye mchakato huu.
Pia kitabu kile hakikuwa matokeo ya maboresho ya rasimu iliyowasilishwa na ndio maana kwa kiasi kikubwa mtagundua kuwa misingi mikuu ya rasimu ya katiba ya Tume ya Rais (Warioba) imevunjwa na kilichomo kimezingatia maoni ya Andrew Chenge na kamati yake kama walivyoagizwa na Samuel Sitta.
Mtakumbuka pia kuwa, mchakato wa kupiga kura bungeni uligubikwa na vitisho, kificho na uvunjaji wa kanuni za Bunge na ulifikia tamati kwa kuchakachua wapiga kura na idadi ya kura zenyewe. Kwa takwimu tulizokwisha toa tangu awali zinaonesha wazi kuwa haikufikiwa theluthi mbili ya kura kutoka Zanzibar, na hivyo kile kilichoitwa Katiba Inayopendekezwa ni batili.
Kwa hiyo basi, juu ya mchakato wa Katiba tunasema:
1. UKAWA unawataka viongozi wetu wote , kuanzia viongozi wakuu wa vyama, Wabunge na viongozi wote ngazi zote kuanzia sasa wafanye Mikutano ya hadhara katika maeneo yao na kuwafafanulia wananchi Mapungufu makubwa ya Katiba Pendekezwa. Aidha, UKAWA utatumia Mbinu mbali mbali ya kuzunguka nchi nzima kijiji kwa kijiji kuwahamasisha wananchi kukataa Katiba Pendekezwa.

2. Tunapenda kuwajulisha wananchi kuwa kuanzia sasa tuko kwenye harakati ya kutafuta Katiba ya Wananchi itakayojengwa katika Misingi ya Maridhiano ya Kitaifa, Katiba itakayobeba matakwa ya wananchi na siyo matakwa ya watawala.
3. UKAWA tutapigania uwepo wa hali ya haki na uhuru kwenye zoezi la kupiga kura za maoni ili wananchi wote wapate nafasi ya kupiga kura. Kama Tume ilivyosema haina Daftari Kamili la Wapiga Kura na inabidi waandikishe Daftari Jipya la Wapiga Kura. Hatutakubali kura ya maoni kupigwa bila Wapiga Kura wote kuandikishwa na Tume ya Uchaguzi.
4. Kuna Vijana zaidi ya milioni 4 waliokuwa na umri wa miaka 13 -17 mwaka 2010 ambao hawajaandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura. Pia kuna watu wengi wamepoteza vitambulisho vya kupiguia kura na wana haki ya kupiga kura ya maoni. Tume ya Uchaguzi haijaboresha Daftari la Wapiga kura kama inavyotakiwa na sheria. Vijana hawa wanajihamasisha kupeleka hati ya kudai haki yao (petition) ya kuipigia kura Katiba Pendekezwa.

3. USHIRIKI WA UKAWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Ndugu wana habari, Kwa kuzingatia jinsi Wajumbe wa CCM wa Bunge Maalum walivyochakachua misingi muhimu ya Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyobeba maoni na dira ya wananchi, ni wazi Katiba ya Wananchi haiwezi kupatikana ikiwa CCM inaendelea kushika hatamu za dola. Kwa yeyote anayetaka kuheshimu maoni ya wananchi na kulinda maslahi yao kuing’oa CCM ni jambo la lazima ili Katiba ya wananchi ipatikane. UKAWA itashirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo asasi za kiraia, viongozi wa dini na makundi mengine katika jamii ambayo yanajiona kuwa ni sehemu ya madai ya Katiba ya Wananchi katika harakati za kufanikisha azma hii.
UKAWA tumeamua kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na tunashiriki kama UKAWA, aidha tutasimamisha wagombea wetu maeneo yote ya nchi kwa umoja wetu. Wagombea wetu watateuliwa kwa kufuata vigezo ambavyo vyama tutakuwa tumekubaliana na pia kwa maoni ya wananchi katika eneo husika.
Aidha vigezo vingine vitavyotumika kupata wagombea na namna ya kuwasimamisha kwa tiketi za vyama vyetu vitatumika kwa maelekezo ya UKAWA kwa kadiri tulivyokubaliana .
Uchaguzi wa serikali za mitaa ni moja ya njia muhimu ya kuelekea kushika dola, na kwetu sisi ni ishara muhimu ya ushirikiano wetu. Hii ni kuwathibitishia kuwa UKAWA ni ushirikiano thabiti na kuwa tumeazimia kwa dhati kuwapatia wananchi njia bora ya ukombozi kuondokana na utawala kandamizi wa chama cha mafisadi.
Aidha tumepitia Kanuni za uchaguzi huu 2014 zilizotolewa na TAMISEMI na kuona mapungufu mengi ila tunahitaji kupata ufafanuzi katika mambo yafuatayo;
i. Idadi ya siku za kuandikisha wapiga kura hazikuwekwa bayana katika kanuni,
ii. Utata kwenye fomu za wagombea na karatasi ya wapiga kura inayohusiana na wao kutakiwa kujaza Nembo ya Chama na Nembo ya Halmashauri,
iii. Utata wa Wananchi wa Kijiji,Mtaa na Kitongoji kutakiwa kuandika majina ya Wagombea na vyama vyao ambao anawapigia kura, na ni Kwanini majina yasiandikwe kwenye karatasi maalum za wapiga kura ili iwe rahisi kwa mpiga kura kuweka alama ya vema kwa majina anayoyapigia kura.
iv. Kwanini muda wa mwisho wa Kampeni uwe saa 11 jioni Wakati kwa utamaduni wa nchi yetu na sheria ya Vyama vya Siasa inaweka wazi kuwa muda wa mikutano ya kisiasa ni saa kumi na mbili jioni. Hata wakati wa uchaguzi mkuu mikutano hufanyika mpaka saa 12:30 jioni. kulingana na Jiografia ya maeneo husika.

5. KUSAINI MAKUBALIANO “MOU” BAINA YA WANACHAMA WA UKAWA 26/10/204
Tunapenda kuwafahamisha umma wa watanzania kuwa mnamo tarehe 26/10/2014 tutasaini makubaliano ya pamoja kama wanachama wa UKAWA kwenye mkutano wa hadhara ambao utafanyika Dar Es Salaam. Makubaliano hayo yanalenga kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya pamoja kwa ajili ya kujenga taifa imara .
Hivyo basi tunapenda kuwaalika wananchi wote kwenye Mkutano huo. Pia taasisi na asasi mbalimbali ambazo zinaona wazi kuwa misingi ya Taifa letu inatikiswa na watawala kwa sababu ya kujaa kiburi na kuendesha nchi kwa hila na ubabe.
UKAWA tuko tayari na tunaahidi kushirikiana na taasisi zote ambazo zinaamini katika kutafuta katiba bora yenye maoni ya wananchi na inayolinda maslahi yao.
Tamko hili limetolewa leo tarehe 18 Octoba 2014 Dar Es Salaam .

Mungu Ibariki Tanzania!
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF
Mwenyekiti CUF
James Francis Mbatia
Mwenyekiti NCCR Mageuzi
Mwenyekiti NCCR Mageuzi
Prof.Abdalah Jumbe Safari
Kny Mwenyekiti CHADEMA.
Kny Mwenyekiti CHADEMA.
Dr. Emanuel Makaidi
Mwenyekiti NLD
Mwenyekiti NLD
Dr. Wilbrod Peter Slaa
Kny Makatibu Wakuu, UKAWA.
Kny Makatibu Wakuu, UKAWA.
0 comments :
Post a Comment