TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Uingereza.
Mchezaji wa Manchester United na Nahodha wa Timu ya Uingereza, Wayne Rooney amemwagia sifa winga hatari wa Real Madrid na timu ya taifa la Ureno Christiano Ronaldo na kusema kuwa ana nafasi kuwa ya kutetea tuzo yake ya mchezaji bora wa Dunia (Ballon d'Or) Mwaka huu.
Rooney na Ronaldo waliku pamoja katika kipind cha mafanikio kwa miaka mitano kabla ya Mreno huyo kujiunga na matajiri wa Hispania kwa dau lililovunja rekodi la £80milioni.

Etihad
Kocha wa Manchester City Manuel Pllegrini huenda akawekwa kitimoto baada ya kupokea kipigo kingine nyumbani hapo jana, na kufanya timu hiyo iendeleze wimbi la rekodi mbaya katika ligi ya mabingwa wa Ulaya.

Man City ilipokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa CSKA ya Urusi, huku wakishuhudia kiungo wao mahiri Yaya Toure akionyehswa kadi nyekundu katika mchezo huo, na winga wao David Silva akiambulia majeruhi ya mhuu wake.

Kapteni wa mabingwa hao watetezi, Vicent Cmpany amesema bado anaimani na timu hiyo, japo hilo si sababu ya uongozi wa juu wa timu hiyo kuwa na mashaka na kocha Pellegrini.

Anfield
Na kocha wa Liverpool amesema bado ana imani na mshambuliaji wake Mario Balotelli ambaye hajaonyesha makali yake msimu huu baada ya kusajiliwa kutoka klabu ya AC Milan ya Hispania.

"Tulimnunua (Balotelli) ili tumpe nafasi, na tutampa kila nafasi" Alisema Rodgers katika mkutano wa waandishi wa habari, ambaye pia amewekwa kitimoto na mashabiki wa timu hiyo baada ya klabu yake kuvurunda msimu huu.

Ujerumani. Beki wa Bayern Munich ya Ujerumani, Jordi Alaba ameumia goti lake vibaya hadi kupelekea kufanyiwa upasuaji wa mguu utakaomueka nje kwa kipindi kirefu.

Alaba alipata majeraha hayo wakati akiitumikia klabu yake katika ushindi walioupata katika ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Roma Jana.

Klabu ya Bayern Munich imethibitisha hilo kupitia mtandao wake rasmi wa Twitter na kumalizia kwa 'Harsh Tag' ya #GetWellSoon

Ufaransa. Na mshambuliaji wa wababe wa Ufaransa klabu ya PSG Edison Cavani jana alifunga goli la mapema zaidi katika historia ya mechi za ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa kutumia sekunde 38 tu kuuweka mpira kimyani.


Goli la Cavani lilikuwa la pekee katika mechi hiyo, hivyo kuipa PSG ushindi finyu wa goli !-) na kuendeleza rekodi nzuri ya kutokufungwa katika lihi hiyo


 

0 comments :

 
Top