Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad ameshangazwa na Rais Jakaya Kikwete kukumbatia watu wasio na chembe ya sifa ya kuwa waziri.
Dr Slaa amesema ni aibu kubwa kuwateua Samwel Sitta na Willium Lukuvi kuwa mawaziri huku ikijulikana hao ndiyo walioshirikiana kuharibu kabisa mchakato wa Katiba mpya ndani ya Bunge Maalum la Katiba.
Samwel Sitta alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba huku William Lukuvi akiwa Waziri OWM Sera,uratibu na Bunge.Kwa kushirikiana hawa waliharibu kabisa mchakato wa Katiba mpya na kuufanya mchakato wa Katiba ya CCM.Huku Samwel Sitta akiishia kuwaporomoshea matusi maaskofu waliokuwa wakipinga mchakato huo.
Dr Slaa anayerarajiwa na wengi kuwa Rais wa Awamu ya tano ameshutumu pia uteuzi wa Anne Kilango kuwa Naibu Waziri wa Elimu huku ikijulikana ana kashfa ya kuuza kiwanda cha Tangawizi katika jimbo la Same Mashariki.
0 comments :
Post a Comment