Mgombea urais kupitia
chama chaNational Resistance
Movement (NRM), Yoweri Museveni ameahidi ruzuku kwa wakazi wa wilaya ya Wakiso
itakayotumika katika kuleta maendeleo katika eneo hilo.
Museveni pia
amewahakikishia Waganda kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani na kwa wale waliona
mpango wa kuvuruga amani atawasambaratisha ndani ya muda mfupi.
Pia Museveni amewaambia
wafuasi wake kwamba serikali yake itapambana na tatizo la rushwa na kuwashughulikia mara moja wale wote wafujaji wa rasilimali za
taifa katika kipindi chake cha uongozi.
Kuhusiana na masuala ya ukosefu wa ajira kwa vijana, amelaumu
ukosefu wa ujuzi pia ameahidi kutoa shillingi billioni 500 kwa kusaidia vijana
wasiokuwa na ajira na pia kujenga taasisi ya kiufundi katika kila jimbo nchini
Uganda.
Source ( Gazeti la Daily
Monitor) toka nchini Uganda.
0 comments :
Post a Comment