Kenya huenda ikajiondoa kwenye
mashindano ya Olimpiki yaliyoratibiwa kufanyika Brazil endapo hakutakuwa na
suluhu dhabiti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Zika.
Mwenyekiti wa kamati ya olimpiki ya
Kenya bwana Kipchoge Keino amenukuliwa akisema kuwa taifa hilo bingwa wa dunia
katika riadha huenda likajiondoa ilikuzuia kuhatarisha maisha ya wanariadha
wake wasiambukizwe maradhi ya homa ya Zika ambayo imeenea nchini Brazil.
Ugonjwa huo wa Zika ambao huambukizwa
na mbu husababisha madhara mabaya kwa watoto ambao huzaliwa wakiwa na ubongo mdogo zaidi ya kawaida.
''Hatuwezi kuwapeleka wanariadha
wetu Brazil iwapo mlipuko wa ugonjwa wa Zika hautadhibitiwa'' alisema Kipchoge
Keino.
Juma lililopita shirika la Afya
Duniani WHO lilitangaza hali ya tahadhari kwa umma kufuatia
kuenea kwa virusi vya Zika hadi Marekani na mabara mengine.
Vilevile ugonjwa huo ulizua taharuki
baada ya kupatikana kwenye manii mate na hata kwa jasho ya mtu aliyeambukizwa.
Hakuna dawa yeyote ya kutibu ugonjwa
huu kwa sasa wala hakuna kinga ila kuzuia usiumwe Brazil imekuwa ikisisitiza kuwa
ugonjwa huo hautaathiri wanariadha na mashabiki watakaohudhuria
mashindano hayo ya olimpiki yaliyoratibiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu.
Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC,
imesema kuwa inaendelea kushauriana na kamati andalizi ya Rio2016 kwa nia ya
kutathmini tishio la kuenea kwa ugonjwa huo.
Brazil imesema kuwa maeneo
yatakayotumika katika mashindano hayo ya Olimpiki yatakuwa yakichunguzwa kila
siku hadi wakati wa mashindano hayo.
Kenya ndio bingwa mtetezi wa riadha
duniani na iwapo itajiondoa kutoka kwenye mashindano hayo basi athari yake
itakuwa wazikatika riadha.
source: bbc swahili
0 comments :
Post a Comment