
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatarajiwa kuzindua visima sita vya maji katika jimbo la Kyela.
Akizungumza na wanahabari kiongozi wa Chadema Kyela na Mjumbecwa mkutano mkuu amesema visima hivyo vimefufuliwa na Chadema mara tu baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa Vijiji na kufanikiwa kuongoza halmashauri ya mji wa Kyela.
Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe na CCM yenye madiwani wengi walishindwa kufufua visima hivyo kwa madai hamna hela kutokana na ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Halmashauri hiyo.
Dr Slaa amealikwa kuzindua visima hivyo kutokana na maombi ya wananchi wa Kyela ambao wana imani kubwa Dr Slaa ndiye atakayekuwa Rais wa awamu ya tano.
0 comments :
Post a Comment