Siku kadhaa sasa zimepita tangu nguzo moja kati ya nguzo zinazoshikilia nyaya za umeme idondokee nyumba na kubomoa ukuta na kusababisha uharibifu mkubwa.
Ni mara kadhaa wanakikijiji wa mtaa wa Chikundi kijiji cha Nkowe wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wamekuwa wakiutaarifu uongozi wa shirika la Tanesco wilayani humo juu ya tatizo la nyaya kushuka bila mafanikio yoyote.
Kwa sasa nyaya hizo zimeshuka na kubakiza urefu wa futi 3 tu kufikia chini ambapo mtu yeyote akitaka kupita chini ya nyaya hizo analazimika kuinama ili kukwepa kugusana nazo.
Wanakijiji wameizungumzia hali hiyo kama ni uandaaji wa maafa makubwa ambayo yanaweza kutokea kijijini humo kama wahusika hawatakuja kushughulikia.
0 comments :
Post a Comment