Wakuu naombeni ushauri labda unaeza kumbadilisha mama yangu mzazi
Mama kawa ni mtu asiesikia baada ya kuokoka tangu mwaka 1995 huko nyuma alikua sio sana kiasi kwamba hata biashara alikuwa anafanya.
Cha ajabu baada ya baba kuhamishiwa Dar kikazi amekutana na kanisa tofauti na lile alilokuwa akisali, wakuu mama yangu anaenda kanisani kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa tatu.
Hajui wadogo zangu wawili wamekula nini wameoga na wako wapi, imefikia baba kutoka kazini na kupika. Cha ajabu hata akipewa hela ya mtaji yote anapeleka kanisani hajui mme ni nini amekula. Kashauriwa na kila mtu hadi bibi na babu waliomzaa ila habadiliki mpaka baba kathubutu kusema ana mchepuko na ndio unaompa furaha hapa duniani.
Sasa wakuu je, hata kama ni kumuomba Mungu kweli hata kusahau majukumu yako kama mama kumsahau mume wako hata hela ya matumizi ya kula unapeleka kanisani. Nathubutu kusema mama nahisi anapepo na nina mashaka na hilo kanisa kwani mama kazeeka sana kaisha jamani
0 comments :
Post a Comment