Hivi karibuni “actress” grade bongo, Kajala masanja ambaye pia ni
mzazi mwenzie na producer P Funk Majani aliandika waraka mrefu
“Instagram” kuelezea ni namna gani anaumizwa na ugomvi uliopo kati yake
na Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa mahojiano aliyokuwa akifanya Kajala mara kwa mara,
alidai kuwa yupo tayari kusuluhishwa na amekuwa akijishusha mara kadhaa
kum”beg” Madame.
Post aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa IG mama Paula jana usiku,
imetafsiriwa na fans pamoja na followers wake kama dongo kwa Wema Sepetu
baada ya kudai amejishusha amechoka, kauli ambayo imeonekana ni katika
kule kuchoshwa na kujishusha ili kutafuta suluhu ya tatizo lao.
“siku zote ukikimbizana na chizi nawewe utakua chizi!!! nimejishusha nimechoka” ameandika Kajala.
0 comments :
Post a Comment