TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Taasisi isiyo ya kiserikali CHESO, imeomba serikali ijayo kuzingatia adhabu za kifungo cha maisha na kunyongwa kwa watu walio kwenye makundi maalumu.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mkurugenzi wa CHESO, Richard Shilamba, alisema kuwa sheria zilizopo hazielezei wazi juu ya watu walio kwenye makundi maalumu juu ya baadhi ya adhabu ambazo kwa upande mwingine zinawakandamiza na kuwanyima haki za msingi kwao.
Alieleza kuwa makundi hayo ni kama vile, wakina mama wajawazito, wakinamama waliojifungua, watoto, watu wenye ulemavu wa ngozi na familia za wahukumiwa wa kifungo cha maisha na kunyongwa.
Akilezea kwa upande wa watoto waliochini ya umri wa miaka 18 alisema kuwa watoto wengi huwa wanahukumiwa kunyongwa ikiwa hali halisi hawajafikisha miaka 18 au miaka 18 hiyo imewakuta wakiwa gerezani.
kwa upnande wa kina mama waliotoka kujifungua, wao sheria haiwaondoi katika adhabu ya kunyongwa, wakati mama anatakiwa kunyonyesha mtoto kwa miaka miwili, hivyo sheria haimpi haki mtoto ya kunyonya kwa kipindi ambacho kinashauriwa na wataalamu wa afya.
Lakini pia taasisi iliangalia kwa upande wa familia za wahukumiwa wa kifungo cha maisha na kunyongwa, kutoruhusiwa kutembelea ndugu zao na kutopewa nafasi ya kupewa miili ya wafungwa hao wanapokufa au kunyongwa kitu kinachopelekea kukosa baadi ya nyaraka za msingi kama vile cheti cha kifo na kufuata taratibu za kimila kulingana na jamii husika. 
Waliendelea kusisitiza kuwa kukosa cheti cha kifo huwasababishia ugumu wa kufuatilia milathi na mambo mengine ambayo yatahitaji cheti cha kifo.
Pia wameitaka sheria kufuata taratibu kama za nchi nyingine ambazo zinaelezea wazi idadi ya miaka ambayo itachukuliwa ni sawa na  kifungo cha maisha kama vile ilivyo kwa nchi kama Brazil ambazo zinaonyesha kuwa kifungo cha maisha ni miaka 20.

0 comments :

 
Top