Moshi. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amesema ndani ya CCM wapo watu wa hovyo, wezi na wanafiki, lakini kama watamchagua Dk John Magufuli kuwa rais, ataisafisha CCM na Serikali yake. “CCM tumejitahidi kuleta maendeleo, lakini lazima nikiri ndani ya CCM kuna kasoro. Tuna mijitu hovyo, tuna wezi, tuna majambazi humo na kuna watu wanafiki ndani ya CCM,” alisema Kinana.
Kinana alitoa kauli hiyo jana mjini Moshi katika mkutano mkubwa wa hadhara wa kuzindua kampeni za ubunge katika Jimbo hilo, ambapo Davis Mosha anapeperusha bendera ya CCM.
“Magufuli atakisafisha chama akiwa mwenyekiti... si mjumbe, lakini anakijua chama.... CCM kuna majungu na ulaji, lakini Magufuli atayamaliza, hajatumia fedha kupata urais, hajaenda wilayani ama mikoani bali alienda matawini.
“Hana makundi... wapo waliochangisha fedha wamekusanya watu baadaye wanakuja kuwa mzigo. Yeye hana makundi wala hana mzigo,” alisema Kinana.
Alisema kuna watu wamefanya uozo ndani ya Serikali na ndani ya CCM na kuamua kukimbia na huko waliko wanasema wataleta mabadiliko wakati wameshindwa kufanya lolote wakiwa madarakani.
Source Mwananchi
0 comments :
Post a Comment