TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dr Wilbrod Slaa, leo amesema kuwa anaachana na kuwa mwanachama wa chama chochote kile na kuwa raia mpiganaji wa haki za watanzania kwa kuwa bado anauchungu na watanzania na mstakabali wa maisha yao.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari. Amesema kuwa yeye ameamua kuachana na siasa baada ya chama chake alichokuwa anakitegemea kwa kupigania maadili ya viongozi na kufuata kanuni na taratibu, kukiuka misingi yake na kuruhusu viongozi waliokuwa wakiukwaji wakubwa wa kimaadili kuwa wanachama wa chama hicho baada ya kutemwa na CCM.
Ameeleza kuwa sakata la kumpokea Lowassa ndani ya CHADEMA lilikuwa na mjadala mlefu na wenye misimamo ya kutofautiana, yeye alikuwa hakubaliani na utaratibu wa kumpokea kiongozi huyo na kumpa nafasi ya kupeperusha bendera ya CHADEMA katika uchaguzi wa urais kwa mwaka huu kwakuwa si mchafu.
"si kweli kwamba nilikubali mwanzo kumpokea Lowassa, bali nilikuwa nakataa tangu mwanzo na kumtaka atueleze ukweli juu ya sakata la RICHMOND, lakini hakufanya hivyo na ndipo na nikaamua kuandika barua ya kujiuzuru ndani ya kikao hicho hicho cha kamati kuu na ikachanwa na Profesa Safari nikaandika ya pili." Alieleza Slaa.
Pia aliongeza kuwa maamuzi aliyoyafanya ni maamuzi binafsi na hayalazimishwi na mtu kama wemgi wanavyosema kuwa mke wake ndiye amekuwa chachu ya ,maamuzi hayo.
Alisema kuwa CHADEMA kuchukua viongozi kutoka CCM ambao wametemwa na chama hicho katika uteuzi, CHADEMA ilikiuka utaratibu iliojiwekea wa kupata viongozi ambao ni asset na watakuja mapema kabla ya mchakato wa kura za maoni ili pia wapatiwe mafunzo kama yeye alivyokuwa ameahidi kwa wabunge wote kuwapatia mafunzo.
Kwa upande wa sakata la RICHMOND, Dr Slaa alisema kuwa yeye analifahamu sakata hilo kiundani kwani yeye 2008 alikuwa mbunge na alikuwa kati ya wabunge ambao walijaribu kurubuniwa ili kukaa kimya kwa kushawishiwa kupewa kitita cha Milioni 500, ambazo alizikataa.
"ubaya wa watanzania hatutaki kusoma, someni maadhimio ya kamati ya Mwakyembe, ambayo yalimtaka waziri kujipima yeye mwenyewe au bunge lijadili na liamue juu ya hatua gani Waziri mkuu achukuliwe. Hivyo basi namuomba Lowassa ajitokeze hadhalani aseme wakubwa hao ni wakina nani wanaohusika na si kusema kipropaganda, kwani wakubwa wako wengi"
Alieleza kuwa mpaka sasa yeye si mwanachama wa chama chochote kile bali anaendelea na mapambano kwa watznania kwani hata yeye ni mtanzania na anazijua sheria za nchi na uhuru wake wa lutoa maoni.
Pia amewataka watanzania wasijerudia kosa la kuchagua kama walivyoafanya kipindi cha 2010 kwa kuangalia tu maneno mazuri ambayo yamewagharimu maisha yao wenyewe.

0 comments :

 
Top