
“Nimekuwa nikifuatilia kampeni zinazoendelea nchini. Ukawa wametia fora
maana wameonyesha ustaarabu, utulivu na heshima kwa nchi yetu. Kwa
bahati mbaya, CCM ambayo ilikuwa ni chama changu, tangu walipoanza
kampeni wanafanya maajabu na vituko. Walianza kampeni za matusi ya
kustaajabisha. Licha ya CCM kuwa na sera nyingi, lakini hawazungumzii
sera. Wanazungumzia mtu. Ukiona kila mtu anamzungumzia mtu mmoja, tena
huyo huyo... jua kuwa mtu huyo atakuwa ni mzito sana. Siasa si uadui.
Nimewaacha CCM kwa sababu siwezi kukubaliana na uongozi unaovunja katiba
za chama, taratibu za chama na unaowadhalilisha wagombea wa urais. Kila
mtu ana haki ya kumchagua rais anayemtaka” .alisema hayo Kingunge
alipopanda jukwaa la UKAWA hapo jana
0 comments :
Post a Comment