Mtatiro akimkabidhi zawadi mgombea udiwani kata ya Tabata, Asenga, aliyoshinda kwnye mnada uliofanyika kwenye harambee ya kuchangia kampeni za jimbo la Segerea. |
JANA timu ya ushindi ya mgombea ubunge wa jimbo la segerea anayeungwa mkono na vyama vinavyoundwa UKAWA, Julius Mtatiro, ilifanya harambee ya kuchangia kampeni za jimbo la Segerea kwa wiki hii ya lala salama.
Katika hafla hiyo jumla ya milioni 7,280,000 ilipatikana kutoka kwa wadau mbalimbali waliochangia. Bado Julius Mtatiro anahitaji mchango wako kutokana na kazi ngumu aliyonayo ndani ya siku hizi zilizo baki iliatoe elimu juu ya upigaji kura kwa upande wa ubunge katika jimbo lake baada ya Tume ya uchaguzi kulirejesha jina la mgombea wa CHADEMA katika karatasi la kupigia kura wakati mgombea huYo alikuwa amejitoa na kuamua kumuunga mkono Mtatiro kama UKAWA ilivyokuwa imependekeza.
Ukitaka kumchangia Mtatiro, unaweza kuwasiliana na Julius Mtatiro 0787536758 au Rehema Msami 0713453380.
Mungu akubariki na tuendelee na utoaji elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa kuwaambia wanasegerea kuwa wakimpigia kura mgombea ubunge wa jimbo la Segerea kupitia CHADEMA, kura zao zitakuwa zimeharibika, kwani ameshajitoa katika kinyang'anyilo hicho, ni hila tu za Tume ya uchaguzi kutaka kura UKAWA zigawanyike.
Hii picha ilipigiwa mnada wa nguvu na hatimaye huyu ndiye mshindi. |
Mzazi wa mgombea ubunge jimbo la Segerea Julius, akimpa baraka za ushidi mtoto kijana wake |
0 comments :
Post a Comment