TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Chama cha wananchi (CUF), kimesema hakikushiriki kikao cha jana cha UKAWA kutokana na sababu za kikatiba za ndani za chama hicho kwa sababu wao kama chama bado wanajadiliana ili kuafikiana kwa maslahi mapana ya taifa.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara Mhe. Magdalena Sakaya amesema kwa sasa wamekuwa na vikao vinavyojadili kwa upana juu ya namna watakavyogawana madaraka endapo wakishinda uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Sakaya amesema wanachikifanya ni sawa na vyama vingine vinavyofanya na kukanusha kuwa sio kweli kwamba CUF wamejitoa katika umoja huo.

0 comments :

 
Top