TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Aliyekamatwa na milion 700 Dodoma arudishiwa pesa zake, polisi yasema alikwenda Dodoma kununua nafaka
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekanusha taarifa zilizozagaa kuhusiana na Raia wa Asia kukamtwa na fedha zaidi ya sh. m.700 kwa madai ya kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ili wamchague mmoja kati ya waliokuwa wanawania nafasi ya Urais
Polisi imesema kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo

0 comments :

 
Top