Mgombea ubunge jimbo la Segerea kupitia CUF, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA, Julius Mtatiro, amesema jambo la kwanza atakaloanza nalo bungeni atakapoapishwa ni kushughulikia bonde la mto Msimbazi.
Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa kata ya Vingunguti jimbo la Segera leo. Amesema yeye na wabunge wenzake wa UKAWA wa jiji la Dar es salaam, watapeleka hoja binafsi ya kulishughulikia bonde la mto Msimbazi ili lisilete madhara zaidi.
Ameongeza kuwa anashangaa mgembea urais wa CCM kuhutubia eneo hilo la vingunguti na kuondoka bila kulitolea ufafanuzi wa tatizo la bonde hilo.
"Hii ni ishara tosha ya kuwa hazifahamu shida zenu, ndio maana hata kuwaambia ni jinsi gani atatatua kero ya bonde la mto msimbazi kuzidi kubomoka ameshindwa kabisa na kuondoka. Ndio maana nikawaambia UKAWA kupitia CUF kwa jimbo la Segerea pamoja na rais ajaye Edward Lowassa kupitia chadema, ndio suruhushi la matatizo yenu, kwani tunayajua matatizo yenu" Amesema Mtatiro.
Fatuma Mcharuko, kutoka Jahaz Modern Taarabu akitoa hamasa kwa wananchi wa Vingunguti. |
0 comments :
Post a Comment