Mgombea mwenza wa urais UKAWA Juma Duni Haji |
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya
upinzani vimedai kubaini mchezo mchafu ambao unataka kufanywa na
serikali ya CCM kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Hali hiyo imejitokeza kutokana na kile kinachodaiwa kuwa NEC imetoa takwimu za upotoshaji ambazo zinalenga kuwapa ushindi CCM na kutimiza adhima yao ya ushindi wa goli la mkono.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) kwa mwanvuli wa Ukawa, Juma Duni Haji alipokuwa
akizungumza na waandishi mjini hapa.
Mgombea huyo alisema kuwa takwimu zilizotolewa na NEC hazina ukweli
wowote na kuna kila sababu ya kutolewa ufafanuzi takwimu hizo
wamezipataje.
Amesema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi inaonesha watu ambao
wanastahili kupiga kura ni milioni 23.7 na vituo vyote vya kupigia kura
vitakuwa ni 72,000 na kila kituo kitakuwa na watu 450.
Amesema katika kufanya ujanja ujanja NEC inaonekana kuwa na wapiga
kura hewa milioni tisa ambapo kuna vituo hewa 20,000 kwa ni vituo halisi
vinatakiwa kuwa 53,000 na siyo 72,000.
Mbali na hilo Haji alifafanua kuwa kwa hesabu ya kuwa na vituo 72,000
kama hesabu ya Tume inavyoelekeza ni wazi wapiga kura wanatakiwa kuwa
milioni 32 na siyo milioni 23 tena.
Kutokana na hali hiyo Duni amemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
Jaji Damian Lubuva kuhakikisha anatoa mchanganuo mzuri wa mahesabu ya
wapiga kura vituo utoa.
“Kamwe hatuwezi kukubali tume kwa kushirikiana na serikali kutafuta ushindi wa goli la mkoni kama ilivyozoeleka kwa chama hicho.
“Hata hivyo natahadharisha serikali ikilazimisha kutaka inachokitaka
wao, bila kusikiliza watu wanataka nini, ni wazi kuwa kunaweza kutokea
machafuko kwani watanzania kwa sasa wamechoka na wanataka mabadiliko,”
alisisitiza Duni.
Akizungumzia kuhusu safari zake, amesema mpaka sasa kafanya mikutano
katika majimbo 130 ambayo mengi yao yapo vijiji na watanzania
wanamalalamiko yanayofanana.
Amesema wananchi wamechoshwa na manyanyaso kwani wamekuwa wakimbizi
katika nchi yao na mbaya zaidi wananyanyaswa na wazawa wenzao na wala
siyo wageni.
Amesema watanzania wamechoshwa na mipango isiyokwisha ambayo
uchangishwa kwa lazima bila kuona mabadiliko yoyote ya ambayo wanatakiwa
kuyapata.
Almesema watanzania wengi wanakumbwa na huduma mbovu ya afya, elimu,
miundombinu, ukosefu wa walimu mashuleni pamoja na shule nyingi kukosa
madawati.
Mbali na hilo alieleza kuwa amebaini kwamba wanachi wengi hawana
uhuru kwa kufanya kile wanachokitaka kutokana na watawala wengi
kuwatisha wananchi.
“Inasikitisha jinsi askari wanyama pori wanavyowashambulia wananchi
hususani wale wanaoishi karibu na hifadhi jambo ambalo linaanyima haki
wananchi kufanya maamuzi,” amesema Duni.
Source Mwanahalisionline
0 comments :
Post a Comment