TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Elimu ya unajimu (astrology)  ina mambo mengi. Kuna numerology inayohusu namba, kuna prediction inayohusu utabiri na kuna palm reading inayohusu kusoma viganja, elimu ambayo leo tutaifundisha na kuona jinsi ya kusoma alama za kiganjani mwako.
Katika mkono wa binadamu, sehemu ya kiganja kuna alama nyingi tofauti ambazo zina maana mbalimbali katika kuelezea tabia ya mtu au mwenedo wake kimaisha.
Alama ambazo ni muhimu sana na ambazo kila binadamu anazo nimeziandika kialfabeti kuanzia A hadi N kama zifuatazo;
Ikiwa mkono wako utakuwa na alama ambayo imekaa kama mnyororo, mtu huyo atakuwa ni mdhaifu, asiye na uamuzi na mwenye tabia ya kuwa na bahati mbaya.
Ukiwa na mstari ambao mwisho umejigawa kama uma, mtu huyo atakuwa ni mbishi mwenye dhamira tofauti.
Ukiwa na mistari miwili ambayo inayoenda sambamba kutoka chini ya kiganja mtu huyo atakuwa ni mwenye kulazimisha mambo na mwenye kupenda kutumia nguvu.
Ukiwa na mistari ambayo imeungana na kuweka kama kisiwa katikati yake mtu huyo atakuwa ni mwenye kufadhaika, dhaifu na mwenye kukata tamaa haraka.
Ukiwa na mstari uliokatika mtu huyo atakuwa ni mtu mwenye kuingiliwa sana katika maendeleo ya maisha yake.
Ukiwa na Mistari midogomidogo inayokatiza mstari mkubwa wowote ni ishara ya upinzani na vikwazo.
Ukiwa na alama iliyokuwa kama msalaba, utapata mshtuko au mageuzi ya ghafla katika maisha yako na alama hiyo ikiwa mwisho wa mstari ni ishara ya kushindwa kimaisha.
Ukiwa na alama ya nyota utakuwa ni mtu mwenye kutokewa na mambo ya ghafla ambayo yanaweza kuwa ya ushindi au balaa. Mkono ukiwa na alama nyingi za nyota ni ishara ya kuwa na maisha ya kusisimua na yenye matukio mengi.
Ukiwa na alama ya mraba ni ishara ya kuwa na ulinzi na mambo mazuri yenye mwelekeo na kuyashinda mambo mabaya yasiyo na mwelekeo.
Ukiwa na alama ya pembe tatu ni ishara ya kuwa mpatanishi, mwenye kupenda amani na utapata bahati nzuri.
Ukiwa na alama ya mstari wenye ncha tatu hiyo ni ishara ya kupata bahati nzuri.
Ukiwa na alama ambayo inafanana na wavu hiyo inaashiria kuchanganyikiwa kimaisha au unakuwa mtu asiye na mwelekeo na asiye na uhakika na asiyejiamini.
Ukiwa na alama nyeusi kama doa au baka unakuwa ni ishara ya mtu mwenye kupenda upatanishi na mwepesi katika makubaliano.
Ukiwa na alama ya duara ambayo ni nadra sana kuonekana katika mikono ya watu wengi, utakuwa ni mwenye bahati kubwa.


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

0 comments :

 
Top