TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Serikali ya Burundi imeamua kusitisha matangazo ya Radio na TV nchini humo kama hatua ya kukomesha maandamano ya wanananchi wanaoshinikiza Rais Nkurunziza kutojiongezea muda.

Vyombo vya habari nchini Burundi, vinashutumiwa kuripoti na kutangaza moja kwa moja maandamano yanayo endelea maeneo mbali mbali jijini Bunjumbura.

Waandamanaji wameendelea kusisitiza kwamba Rais asipotangaza kwamba hagombei tena, wataandamana hadi Ikulu. Waandamanaji wanawachukia Polisi na Kuwapenda Wanajeshi. Wanasema Polisi ndio wanawapiga lakini wanajeshi hawawapigi. Hivyo waandamanaji wanapo waona wanajeshi huwapigia makofi.

Rais Nkurunziza alijiongezea muda wa kugombea baada ya muda wake wa kua rais kikatiba kuisha. Hali hiyo imesababisha wananchi waanze kuyakimbia makazi yao kwani wanakua huo ndo mwanzo wa machafuko Burundi.

Hadi sasa Rwanda imepokea wakimbizi zaidi ya 17,000 kutoka Burundi.

Video ya maandamano

https://www.youtube.com/watch?v=qp5rMlx8L9k

0 comments :

 
Top