Rais wa Marekani Donald Trump anayeondoka madarakani ametoa hotuba yake ya mwisho kuwaaga Wamarekani huku akisema, walifanya kile walichokuja kufanya na walipata mafanikio makubwa.
Katika hotuba yake, Trump hakumtaja Biden kama mshindi wa uchaguzi uliopita, lakini alitumia dakika 20 za hotuba yake kuelezea mafaniko ya uongozi wake.
"Tulirejesha nguvu ya Marekani nyumbani na nje ya nchi, dunia inatuheshimu tena, tulijenga uchumi imara katika historia ya dunia hii, tuliimarisha mahusiano yetu nje ya nchi hasa dhidi ya China.
Lakini tumesababisha uwiano katika eneo la mashariki ya kati, hakuna aliyeamini na sasa eneo hilo lina mwamko mpya, najivunia kuwa rais wa kwanza kwa muda mrefu ambaye hakuanza vita vipya" alisema Trump.
Saa chache kabla ya kuondoka kwake, Trump ametoa msamaha kwa aliyekuwa mshauri wake Steve Bannon, ambaye anakabiliwa na mashitaka ya udanganyifu. Tangazo hilo linawadia saa kadhaa kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden.
Trump pia amewahurumia watu wengine zaidi ya 140 saa zake za mwisho madarakani. Miongoni mwa waliosamehewa ni rapa Lil Wayne huku rapa mwingine Kodak Black na aliyekuwa meya wa Detroit Kwame Kilpatrick wakipunguziwa vifungo vyao.
Kwa ujumla watu 73 wamepewa msahamaha huku wengine 70 vifungo vyao vikapunguzwa, taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema.
Bannon, ambaye alikuwa mshauri mkuu wa Rais Trump wakati wa kampeni yake mwaka 2016, alipatikana na hatia mwaka jana kwa makosa ya udanganyifu juu ya kampeni ya kuchangisha pesa kujenga ukuta katika mpaka ya Marekani na Mexico.
Waendesha mashitaka Bannon na wengine watatu walilaghai wengine mamia ya maelfu ya wafadhili kuhusiana na mradi wa “Tujenge Ukuta” kampeni ambayo ilikusanya dola milioni 25. Inadaiwa kuwa Bannon alipokea zaidi ya dola milioni 1 ambazo baadhi ya pesa hizo alizitumia kwa matumizi yake binafsi.
Alikanusha makosa hayo na alikuwa ahukumiwe. Ikulu ya Marekani imesema Bannon amekuwa “Kiongozi muhimu na anajulikana kwa hekima yake katika siasa.” Taarifa hiyo ilisema kwamba waendesha mashitaka walikuwa wamemfungulia mashitaka yenye kuhusishwa na ulaghai kutokana na kujihusisha kwake kwenye mradi wa siasa.
Katika hatua nyingine, idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Marekani kutokana na janga la Corona, sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya 400,000 kwa mujibu wa takwimu za chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Saa chache kabla ya kuapishwa kwake, rais mteule Joe Biden amewakumbuka Wamarekani waliopoteza maisha kutokana na janga hilo. KUJIONEA MENGI ZAIDI BONYEZA HAPA
0 comments :
Post a Comment