TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Joe Biden amekula kiapo na kuwa rais wa 46 wa taifa la Marekani. Biden amekuwa rais rasmi baada ya kuwa amekula kiapo mbele ya jaji wa Mahakama Kuu John Roberts.


Baada ya kula kiapo Biden amelihutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Rais wa Marekani akisema ''hii ni siku ya kidemokrasia''. Siku ya kihistoria na matumaini.
''Marekani imejaribiwa na kunyanyuka tena dhidi ya changamoto. Leo tunasheherekea ushindi si wa mgombea isipokuwa ushindi wa demokrasia''.

''Ninawashukuru watangulizi wangu wa vyama vyote walio hapa hii leo,'' alisema Rais mpya. Marais wa zamani Clinton, Bush na Obama wamehudhuria sherehe hiyo.

Biden amesema alizungumza kwa njia ya simu na Rais Jimmy Carter- ambaye sasa ana miaka 96, na kumpongeza kwa utumishi wake.

Mtangulizi wake, Donald Trump hajahudhuria tukio hilo muhimu, na hatua hiyo imemfanya kuwa rais wa kwanza kutohudhuria sherehe za kuapa kwa mrithi wake tangu mwaka 1869.

Rais Biden ametangaza msururu wa maagizo yanayolenga kugeuza sera kuu za Bwana Trump.

Makamu wa Rais mteule Harris aliapishwa mbele ya Bwana Biden – kuwa mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza mweusi na mwenye asili ya Asia na Amerika aliyeinuliwa kuhudumu katika nafasi ya pili muhimu baada ya Urais.

Shughuli za uapisho zimefanyika wakati kukiwa na ulizi mkali baada ya waandamanaji wanaomuunga mkono Trump kufanya vurugu tarehe 6 mwezi Januari.

Wanajeshi 25,000 wanalinda eneo linalofanyika sherehe hizo, sherehe ambazo zimekosa kuhudhuriwa na maelfu ya watu kama ilivyo desturi yake kwa sababu ya janga la corona. JUA ZAIDI KUHUSU BIDEN NA URAIS WAKE HAPA

0 comments :

 
Top