Didier Drogba, afunguka nakudai anatamani kuwepo tena klabuni Chelsea kwa mara nyingine akiwa kama kocha.
Mshambuliaji huyo wa Ivory
coast anayekipiga katika klabu ya
Montreal Impact kwa soka la kulipwa huko Canada, na ambaye aliifungia “the blues” mabao 164 katika maisha
yake ndani ya Stamford Bridge athibitisha hamu yake ya kurudi Chelsea kama
mkufunzi katika utambulisho wa kitabu chake kiitwacho “Commitment”.
Drogba ambaye bado ni shujaa kwa “the blues” kwani aliifungia
bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012,
amedai kuwa angependa kuihudumia klabu
hiyo hata baada ya kukamilika kwa kipindi chake cha uchezaji.
Muivory coast huyo alithibitisha
kuwa tayari nimekubaliana na Wakurugenzi
wa klabu hiyo kuwa ana uwezekano wa kurejea kuwa mkufunzi kwa sababu klabu hiyo inamfaa
sana.
Tembo huyo pia alizungumzia uwepo wa
uongozi mzuri kati ya wachezaji kwa kumtolea jicho la undani zaidi nahodha John
Terry kuwa yupo pekee yake mkongwe kwa
kudai enzi zao hawakupoteza michezo kirahisi kama sasa ambapo Chelsea imepoteza
michezo 7 kati ya 13 huku wakiwa vnyuma ya Arsenal kwa pointi 12 kwa kuwa
kipindi chao walikwepo wachezaji mahiri wenye nguvu ya ushawishi kama yeye,
Michael Ballack, Andriy Shevnchenko, John Terry, Makelele, Michael Essien na
wengineo.
Kuhusu suala la uongozi alihoji ''Kwani
haiwezekani kuwa meneja? siwezi kuwa mkurugenzi wa kiufundi, mkufunzi wa chuo
cha mafunzo ya wachezaji ama hata mshauri wa washambuliaji? alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37.
Kuhusiana na nafasi ya waliopo Chelsea,
tembo huyo wa Afrika Magharibi amedai
bado kocha wake Jose Mourinho ni “special” kwake kwa uhusiano na na
uwezo alio nao lakini hakusita kumtaja kocha bora aliyewahi kukutana na kupambana na vijana na wake katika
maisha ya soka kuwa Sir Alex Ferguson enzi zake Old Trafford.
Drogba alikwenda mbali nakudai
kikosi cha Arsenal kina uwezekano wa kuchukua ubingwa wa England msimu huu kwa
kuamini rafiki yake Petr Cech waliyecheza nae Stamford Bridge kwa ukongwe atakuwa nafasi nzuri kuchukua
vikombe ndani ya kikosi cha “the Gunners”.
Kwa upande wa timu bora aliyopambana
nayo ni Barcelona huku akiwahusudu Ronaldinho, kiungo wa zamani wa Barcelona na
timu ya Taifa ya Brazil, Lionel Messi na Zinedine Zidane kuwa moja kati ya
wachezaji wa kiwango cha juu aliowatamani kuwa kikosi kimoja na wao.
0 comments :
Post a Comment