Rais wa Marekani Barack
Obama amesaini sheria yenye lengo la kupanua umeme kwa mamilioni ya kaya Kusini
mwa jangwa la Sahara na yenye kuokoa maisha na kuongeza kasi ya ukuaji barani Afrika.
Sheria hiyo ilipitishwa
kwa kauli moja na Baraza la Wawakilishi, Seneti na kwa kushirikiana na sekta
binafsi ambapo watahakikisha upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 50 katika
sehemu ya Afrika.
Serikali ya Marekani
imeahidi kutoa fedha kwa ajili ya mradi
ambao utatumia mfumo wa dhamana ya mkopo kwa kuongezaa megawati 20,000 za umeme
wa gridi ya bara hilo la Afrika ifikapo
mwaka 2020.
Hatua hiyo inatarajiwa kuwa itachochea
ukuaji wa uchumi na kuboresha upatikanaji wa elimu na afya ya umma.
"Familia nyingi zitapumzika
kutumia mkaa au vyanzo vingine vyenye sumu". anadai Mwenyekiti wa
Kamati ya Mambo ya Nje ndugu Royce.
Hatua hii ya Rais Barack Obama ya kusaini sheria ya mradi wa umeme uitwao ‘Power Africa’ ni kati ya ahadi alizotoa pindi alipotembelea nchini Kenya mnamo mwezi wa saba mwaka 2015.
Source (gazeti la Daily
Nation) toka nchini Kenya
0 comments :
Post a Comment