Riyad Mahrez ni winga wa kimataifa wa Algeria alizaliwa miaka
24 iliyopita, mjini Sarcelles nchini Ufaransa mnamo tfebruari 21, 1991.
Alianza maisha yake ya soka katika kituo cha AAS Sarcelles
akiwa na miaka 12 na ilipotimu mwaka 2009 Mahrez alifanikiwa kujiunga na timu ya
Quiemper kama winga na kuifungia magoli mawili kwa msimu mmoja yaani 2009/2010.
Mzaliwa huyo wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria aliamua
kuichezea timu ya Taifa ya Algeria kwa kuvunja miiko ya wachezaji wengi
kuchezea nchi walizozaliwa pasipo kuangalia asili ambapo aliiwakilisha Algeria
kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini Brazili pamoja na mashindano ya
mataifa ya Afrika mwaka 2014. Kutokana na
kiwango alichokionyesha alipata ofa ya kuichezea PSG na Marselle za Ufaransa na kuishia kukubali ofa ya kuwepo
katika klabu ya Le Havre na kusaini mkataba wa miaka mitatu, kuicheza mechi za
mashindano 60 na kufunga magoli 6.
Nyota ilipozidi kung’aa, mwaka 2014 akaangukia mikononi mwa klabu ya Leicester
City ya nchini Uingereza iliyokuwa ikishiriki daraja la kwanza maarufu kama
Championship League (kwa sasa inashiriki ligi kuu), mechi yake ya kwanza
ilikuwa tarehe 25, mwezi wa kwanza 2014 ambapo alichukua nafasi dakika ya 79
akibadilishana na Lloyd Dyer dhidi ya
Middlesbrough ambapo walishinda mbili kwa bila.
Ujio wake kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu ya Uingereza
umekuwa wa Baraka pia kwa klabu yake ya Leicester iliyopanda ligi kuu kwani ipo vyema tangu alipoanza
kucheza ligi kuu tangu agosti 18, 2014 na goli lake la kwanza alifunga dhidi ya
Burnley Oktoba 10, 2014 walipotoka sare ya goli mbili kwa mbili
Msimu wa 2014/2015
umekuwa poa kwake kwa kufunga magoli manne na “ assists” 30, na kusaini
mkataba wa miaka minne klabuni hapo kwa kiwango bora kilichomkuna Mkurugenzi wa
klabu hiyo Nigel Pearson.
Kwa uwezo wake sio mbaya kwa sasa kuwa na goli 14 katika ligi
kuu msimu huu wa 2015/2016 na mpaka sasa
klabu inaongoza ligi kwa pointi 38.
0 comments :
Post a Comment