Bunge la 11 limeendelea
tena Dodoma leo Mei 5 2016, katika kipindi cha Maswali ya papo kwa pako
kwa Waziri Mkuu Mbunge wa Viti maalum (CHADEMA) Dr. Elly Marko Macha alimuuliza Waziri Mkuu
Majaliwa ya kwamba;
“Tanzania ilisaini mkataba wa kimataifa
wa mwaka 2006 kuhusu haki za watu wenye ulemavu, utaratibu ni kwamba baada ya
miaka miwili baada ya kuridhia Serikali inataiwa kuwandika State Report,
Kwanini Serikali haijapeleka hiyo ripoti hadi leo kuhusu watu wenye ulemavu?”
Serikali yetu imedhamilia kufungua milango na
kutoa huduma na kuwafanya ndugu zetu wenye mahitaji maalum kuwa ni sehemu ya
wachangiaji wakubwa wa shughuli za kimaendeleo nchini’
‘Mikataba
hii baada ya kuwa tumeunda Serikali yetu tutafanya mapitio ya kazi zote za
awamu ya nne ambazo zilikuwa zimefikiwa na tuweze kuunganisha mkakati ambao
Rais ameuweka ikiwa ni pamoja na hili ambalo Dk. Macha umelieleza’
“Nikuhakikishie, kwakuwa tayari tunaye Waziri mwenye dhamana ya Watu wenye
mahitaji maalum basi wakati wowote kuanzia sasa jambo hili litakamilika na
nimtake Dokta Abdallah Poss aanze mchakato wa kuwakusanya wadau wote ili
tuanze kuyapitia mahitaji hayo”
0 comments :
Post a Comment