Msanii Snura
aiomba radhi jamii kwa kutoa wimbo na video ya “chura” iliyodaiwa na baadhi ya wadau
pamoja na serikali kuwa haina maadilli
na udhalilishaji kwa jinsia ya kike. Hayo ameyasema leo, Mei 5 katika kikao na
waandishi wa habari akitoa ufafanuzi baada ya hiyo jana, Mei 4 Wizara ya Habari,
Utamaduni, Wasanii na Michezo kuifungua kutokana kudai haina maadili na
zaidi, yeye kufungiwa kujihusisha na muziki mpaka pale BASATA watakapomtambua
kwa kujiandikisha kwenye orodga ya wasanii wanaotambulika.
Katika kikao
hicho na waandishi pia, Snura alijitokeza na meneja wa maarufu kama HK na
kuonyesha cheti rasmi alichopewa na BASATA baada ya kujisajili na kuahidi
kutotoa video ya namna na maudhui kama yale tena.
Msanii Snura kulia na meneja wake (HK) kushoto leo katika kikao na waandishi wa habari.
0 comments :
Post a Comment