TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Je, nikiandikiwa faini na askari kwa hizi faini za kieletrokini halafu nikawa sikubaliani na kosa je nitasaini wapi kwamba sikubaliani au natakiwa kufanyaje?

Ni swali ambalo limeulizwa mara kwa mara hasa kwakuwa, notifikesheni za kieletroniki hazina mahali pa kusaini.

Jibu la hili linapatiikana kwenye kanuni.

Kanuni za tozo la papo kwa papo kieletroniki zilipitishwa na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali No. 30 za mwaka 2015. Kanuni hizi mpya zinarekebisha kanuni za utozaji wa faini papo kwa papo zilizotungwa chini ya kifungu cha 95 cha sheria ya usalama barabarani na kutangazwa kwenye gazeti la serikali Na.257 la mwaka 2011. Na ndio maana unaona karatasi za notification za vitabu zimeandikwa GN 257 of 2011.

Kwa mujibu wa kanuni ya 5(2) ya kanuni za tozo za papo kwa papo za kieletroniki, mtu asipokiri kosa  basi ndani ya siku 7 tangu alipoandikiwa notifikesheni  atatakiwa kuripoti kituo cha polisi kwaajili ya kufikishwa mahakamani.

Na kwa mujibu wa kanuni ya 5(3) kama mtu huyo asipojitokeza ndani ya siku saba, basi itahitimishwa kuwa amekubaliana na kosa, na hivyo kutakiwa kulipa faini aliyoandikiwa pamoja na penati inayoongezeka kutokana na kuchelewa kulipa.

PENATI ZINAZOONGEZEKA BAADA YA FAINI

Je, ni penati kiasi gani inayoongezeka kila unapochelewa kulipa faini ?

Kwa mujibu wa kanuni ya 6(5)(a) na (b) Iwapo mtu atalipa faini kati ya siku 8 na siku 14, basi atalipa kiwango cha faini na penati itakayoongezeka kwa asilimia ishirini na tano (25%). Maana yake ni 30,000 + 25%.

Baada ya kupita siku 14, yaani kuanzia siku ya 15 na kuendelea mtuhumiwa atatakiwa kulipa kiwango cha faini alichoandikiwa awali na ongezeko la penati la asilimia hamsini (50%). Maana yake ni 30,000+50%.

Na iwapo zitazipta siku 30 bila kulipa faini hiyo ya awali pamoja na penati zilizoongezeka, na mtu huyo akatenda kosa jingine basi faini yake sasa itakuwa shilingi elfu hamsini (50,000) au kifungu cha miezi miwili jela, au vyote kwa pamoja faini na kifungo. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 6(6).

Bila kujali kauni zilizotangulia hapo juu, kutakuwa na ongezeko la 50% kwa kila penati mtuhumiwa aliyoshindwa kulipa kwa kila siku 30  za kuchelewa kulipa penati hiyo. Maana yake ni kwamba umeandikiwa kosa moja 30,000, hukulipa ndani ya siku 30, inaongezeka 50%. Unakaa tena unapitisha siku 30 nyingine jumla zinakuwa siku 60.

Hapo inaongezeka tena 50% kwenye ile penati ya 50%. Hivyo kimahesabu itakuwa  siku 30 za kwanza ni 30,000 +15000=45000; siku 30 za pili deni litakuwa 45,000+7500 (Hii 7500 ni 50% ya ile 15000 ya penati ndani ya siku 30)=52,500. Ukipitisha siku 30 nyingine yaani jumla una siku 90, inakuwa 52,500+7500 tena=60,000.

Iwapo hata baada ya kupita siku hizo 90 hujalipa au tangu ulipoandikiwa huonekani kabisa, basi madeni yako utalipa wakati wa kurenew leseni yako.

0 comments :

 
Top