Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia msanii Gigy Money kwa kutojihusisha na masuala ya burudani na sanaa kwa muda wa miezi 6 pamoja na faini ya Milioni 1 kwa kosa la kudhalilisha utu wake kuonesha mauongo yake ya mwili.
Adhabu hiyo inaendana na ya Televisheni ya Wasafi (Wasafi Tv) ambayo ilirusha Video hiyo ambapo nao wamefungiwa miezi 6 na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kurusha matangazo yao.
BASATA wametoa taarifa hiyo kufuatia tukio la msanii huyo kupanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza kisha akavua gauni lake na kubakia na dela, vazi ambalo lilikuwa linaonesha maungo yake ya ndani ya mwili hivyo alibugudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya Tanzania.
Aidha BASATA wameendelea kusema walishamuita msanii huyo kwa ajili ya kumuonya vitendo hivyo vya ukiukwaji wa sheria za maadili na aliahidi kutorudia tena, pia Baraza linawakumbusha wasanii wote hapa nchini kufanya sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu.
0 comments :
Post a Comment