TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Mahakama ya wilaya ya Mvomero imewaachia huru Daniel Naftal Ngogo na wenzake katika Kesi ya Jinai namba 1 ya Mwaka 2020,

Katika kesi hii Washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na Makosa mawili, (I) Kufanya Kusanyiko lisilo halali (II) Kutotii amri halali ya Polisi

Akisoma hukumu hiyo , Hakimu amesema Upande Mashtaka Umeshindwa Kuithibitishia Mahakama Pasipo na Shaka juu ya Watuhumiwa kutenda Kosa katika Mashtaka yote Mawili.

Aidha Hakimu amesema ni KAZI ya Upande wa Mashtaka Kuithibitishia Mahakama namna ambavyo washtakiwa wamehusika katika Mashtaka husika kinyume na Ushahidi Uliotolewa.

Vile vile Mahakama imejiridhisha kutoka kwenye Ushahidi Uliotolewa na Pande zote kuwa Washtakiwa wote ni Viongozi wa CHADEMA wilaya pamoja na Mmoja ambaye ni Afisa kutoka Makao makuu ya CHADEMA, Na pia kweli watuhumiwa hao walikuwa wakifanya Mkutano wao wa CHADEMA eneo la Dakawa kwenye Bar ya Mzee Anae Urio ambapo pia ndipo zilipo Ofisi za CHADEMA Wilaya ya Mvomero. 

Pamoja na hayo hakuna Ushahidi wowote ambao unathibitisha kuwa Watuhumiwa walikusanyika isivyo halali na pia hawakutii Amri halali ya Polisi. 

Hivyo Mahakama imewaachia Huru washtakiwa wote namba Moja mpaka namba 5 ( Daniel Naftal Ngogo/Mrisho Ramadhani/Kashkash Saimanga na Msulwa Donald ) kutokana na kukosekana Ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani.

Taarifa hii imetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro Jackson Malisa, leo January 5, 2020

0 comments :

 
Top