Mwanamke Mkenya amekuwa akipika chakula na kuwapatia Wakenya wenzake wanaoishi katika miliki za kiarabu UAE waliopoteza kazi kutokana na mlipuko wa corona.
Wangeci Waruire alikuwa dereva wa teksi za Dubai na wakati wa usitishwaji wa safari za ndege na kusababisha viwanja vya ndege kufungwa, ndipo kulimfanya kuachana na kazi hiyo kutokana na kipato kushuka cha malipo ya kazi hiyo kwakuwa wateja walipungua kwa kiasi kikubwa, na hivyo kufanya mahitaji yake yasikidhi kwa malipo hayo.
Hata hivyo msaada toka kwa mme wake ulimfanya kupata msukumo zaidi wa kuendelea kuhudumia wenzake hao kwa kuwapa mlo baada na yeye kutokuwa na kazi tena ya kumwingizia kipato.
Mama huyo wa watoto watatu aligundua kwamba watu wengi hawana kazi ndipo sasa akaamua kuwapatia chakula cha bure. Anasema alikuwa akitumia mtandao wa Kenya kuwasiliana nao pale chakula kikiwa tayari kwa kupost kwenye mtandao huo na kuelekeza wapi wanaweza kipata chakula hicho.
Richa ya Wakenya kuwa ndio wenye idadi kubwa ya wahudumiwa, amesema pia watu wa mataifa mengine ya Kiafrika, wamekuwa ni moja ya watu wamekuwa wakijitokeza kupata chakula hicho.
Ametoa rai kwa watu wote kushirikiana katika majanga kama haya kwakusaidia wale ambao wanapitia mkwamo wa kimaisha hasa wa kiajira kama ilivyo wakati huu wa Corona.
0 comments :
Post a Comment