Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Abubakar Kunenge leo Januari 7, 2021, ametembelea ofisi za East Africa Television na East Africa Radio na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji Regina Mengi.
Akiwa ofisini hapo ametembelea sehemu mbalimbali ikiwemo studio za TV pamoja na Radio na kujionea jinsi shughuli za kila siku katika kuhabarisha umma zinavyofanyika.
Kunenge, alipata nafasi ya kujumuika katika kipindi cha MamaMia katika studio za East Africa Radio, ambapo amepongeza jitihada nzuri zinazofanywa na East Africa Radio kupitia vipindi vyake hususani kuhamasisha akina mama pamoja na makundi mengine kushiriki kwenye maendeleo
''Niwapongeze East Africa Radio, watangazaji na uongozi mzima kwa namna ambavyo mnafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Dar es salaam, wanashiriki kwenye shughuli za maendeleo'', - RC Kunenge.
''Kwa mfano hiki kipindi cha MamaMia mnasemea vizuri masuala ya kina mama na sisi baada ya serikali kuhamia Dodoma sasa jiji letu limebaki kuwa la kibiashara na tunayo mikakati mingi na mikubwa kuhakikisha wanawake wanaendelea''. - RC Kunenge.
''Mkoa wa Dar es salaam ni mji wenye fursa nyingi na tunatoa mikopo mingi kwa akina mama mikakati yetu nikuhakikisha tunatangaza biashara katika mkoa huu katoka nchi jirani ili waje hapa'' RC Kunenge
''Tunawapatia akina mama wanaoanzia chini mafunzo na tunaondoa urasimu kwenye upatikanaji vibali vya biashara ili wafanyabiashara wadogo wasiweze kusumbuliwa'' RC Kunenge
''Mikakati kwasasa ni mingi na tunachofanya sasa, tumeamua kutoa vifaa vitakavyowezesha wafanye biashara kwani wengine ukiwapa pesa huwa wanagawana'' RC Kunenge
0 comments :
Post a Comment