WANANCHI wa Kijiji cha Kasheka, Kata ya Bangwe katika Jimbo la Buchosa wamecharuka baada ya viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya vifaa vya ujenzi vinavyoletwa kijijini hapo kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho.
Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Eric Shigongo, wananchi hao wamedai kuwa viongozi wa Kijiji wamekopeshana mifuko mia mbili ya saruji ambayo ililetwa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo na mpaka sasa hakuna aliyerudisha.
“Tunakushukuru Mhe. Mbunge kwa kutuletea mifuko 100 ya saruji, ile zahati imechukua mifuko 250, ukiongeza nay a kwako inakuwa 350, jiandae kutoona chochote pale, usipokuwa makini viongozi wa Serikali ya Kijiji watagawana hiyo mifuko na Zahanati haitokamilika.
“Kuna mifuko ilitolewa pale, viongozi wamekopeshana, wamekuwa na tabia hiyo kwa muda mrefu, mtaendelea kutusaidia mpaka lini. Pia, kuna viongozi wa kata ukienda ofisini na shida wanakutoza Tsh 5,000 inakwenda wapi?” amesema Mzee Adam Mafuru Malogo.
Kwa Upande wake Mhe. Shigongo amesema bahati mbaya waliokuwa nao viongozi hao wa Serikali ya Kijiji ni kwamba mbunge wao ni mjasiriamali, ana fahamu machungu ya kutafuta pes ana matumizi mabaya ya pesa.
“Saruji hii imetoka kwa mjasiriamali, ikipotea hata punji moja ya saruji tusilaumiane, ole wao waitumie vibaya hiyo saruji, wote wataishia Gereza la Kasungamile na hii tabia ya kula mali za umma katika Jimbo hili imefika mwisho, ambao wanabisha wajaribu waone,” amesema Shigongo. BOFYA HAPA KUSOMA MENGI ZAIDI
0 comments :
Post a Comment