TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kupitia kwa Katibu Mtendaji wake, Dkt. Charles E. Msonde limetangaza matokeo ya mitihani ya kitaifa ya upimaji wa maarifa darasa la nne na kidato cha pili na kidato cha nne kwa mwaka 2020.

Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dkt. Charles Msonde, ambaye amesema kiujumla kunaongezeko la ufaulu kwa watahiniwa wa ngazi zote kuanzia darasa la nne, kitldato cha pili nanidato cha nne.

"Kidato cha Nne waliofanya mitihani ni 434,654 waliofaulu ni 373,958 sawa na asilimia 85.84, ufaulu wa kidato cha nne umeongezeka kwa asilimia 5.19 ukilinganisha na mwaka 2019" Dkt Charles Msonde

"Kuna ongezeko la 1% kwa wanafunzi waliofaulu kuingia Darasa la Tano ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana na mikoa iliyoongoza ni Dar es Salaam, Lindi na Arusha" Dkt Charles Msonde



2 comments :

Unknown said... 15 January 2021 at 15:11

Matokeo ya form two mngeyapanga in alphabetical order..

Unknown said... 15 January 2021 at 22:14

Mungu atukuzwe kwa matokeo mazuri, na awabarki waandaji pia kwa kazi nzuri...but Mwalimu akumbukwe kwa mchango wake katika Ujenzi wa Taifa,Maana haya yote ni kazi ya Walimu.

 
Top