Kwa watu waliopanga kununua gari kipindi hiki watapaswa kujikung’uta zaidi mfukoni kutokana na kuongezeka kwa bei hadi Sh3 milioni kwa baadhi ya magari ikilinganishwa na wiki iliyopita.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii suala la kuongezeka bei za magari liliibua mjadala likihusishwa na ongezeko la kodi, taarifa ambao Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) iilikana jambo hilo.
Hata hivyo, wauzaji wa magari katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wamedai kuwepo ongezeko linalotokana na mabadiliko ya kodi na ushuru ambayo yamewekwa na TRA ndani ya wiki moja iliyopita.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo aliliambia gazeti hili kuwa hana taarifa za kuongezeka kwa ushuru katika siku za karibuni na kusisitiza kuwa sheria ya kodi inayotumika ilianza Julai mosi na hakuna mabadiliko mengine.
Aliongeza kuwa “Viwango vya Kodi kwenye sheria ni vilevile. Vinavyoweza kubadilika badilika ni ‘exchange rate’ (kiwango cha kubadilishia fedha) na bei za bidhaa kwenye ‘data base’ (kanzi data) ya dunia ambayo inatumika duniani kote.”
Muuzaji wa magari jijini Dar es Salaam, Hendh Razack alisema bei zimeongezeka kwa sababu TRA imebadilisha kiwango cha wastani wa bei ya gari (Customs Value CIF) ambacho kinatumika kukokotoa kodi. ANGALIA ZAIDI HAPA
0 comments :
Post a Comment