TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na kisha kufanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Bashiru Ally

Mabadiliko hayo ametangaza mara baada ya uapisho wa Makamu wa Rais na kusema kuwa amefanya uteuzi wa wabunge watatu ambao ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Bashiru Ally, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Mabadiliko hayo yamefanya Rais kuwateua wafuatao
• Wizara ya Fedha – Mwigulu Nchemba
• Wizara ya Tamisemi – Ummy Mwalimu
• Wizara ya Muungano – Suleiman Jafo
• Wizara ya Utumishi na Utawala Bora -- Mohamed Mchengelwa
• Wizara ya Mambo ya Nje – Libelata Mulamula
• Wizara ya Katiba sheria – Prof. Kabudi
• Wizara ya Viwanda na Biashara – Prof. Kitila Mkumbo
• Uwekezaji – Geophrey Mwambe
• Kazi Maalum – Mkuchika

• Wizara ya Mifugo, Naibu Waziri – Abdalah Ulega
• Wizara ya Habari, Naibu waziri – Pauline Gekul
• Wizara ya Afya, Naibu Waziri – Mwanaidi Ally Hamisi
• Wizara ya Mambo ya Nje, Naibu Waziri – Mbarouk Mbarouk
• Wizara ya Katiba na Sheria, Naibu Waziri – Geophrey Pinda
• Wizara ya Muungano, Naibu Waziri – Hamad Said Chande
• Wizara ya Fedha na Mpiango, Naibu Waziri – Masauni Hamad
• Wizara ya Uwekezaji, Naibu Waziri – William Ole Tate

Vilevile Mhe. Samia Suluhu amefanya uteuzi wa Wabunge wateule
• Dkt.Bashiru Ally
• Mbarouk Mbarouk
• Libelata Mulamula

Pia Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Hussein Katanga ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Japan kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Balozi Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.

Aidha, Mawaziri wote walioteuliwa leo wataapishwa kesho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.

                      DOWNLOAD APP YETU

0 comments :

 
Top