Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema chama chake kinaunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyotolewa na Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti huyo alikuwa akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji
la Mbeya katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Iyela kwa
tiketi ya Chadema Charles Nkelwa.
Kiongozi huyo wa upinzani bungeni amesema sababu kubwa ya kuunga mkono
rasimu hiyo ni kwamba mambo mengi yaliyoorodheshwa na chama hicho
yamekubaliwa.
Mbowe amesema jambo kubwa lililofanyiwa kazi ni kurejeshwa kwa serikali
ya Tanganyika. Mbowe amesema amesikitika kuona baadhi ya wanaCCM
wakiipinga serikali ya Tanganyika na kung'ang'ania serikali mbili na
kudai watu hao ni wanafiki wanaopaswa kupuuzwa na wananchi.
Kauli ya Mbowe imekuja wakati ambapo mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dr
Kitila Mkumbo alinukuliwa kusema rasimu mpya ya Katiba iliyotolewa na
Warioba ni bora mara mia mbili akilinganisha na katiba ya sasa.
Mara baada ya mkutano huo maelfu ya watu walitanda barabarani kumsindikiza kiongozi huyo anayependwa sana jijini Mbeya.
Source: Mwananchi Jumatatu.
Home
»
»Unlabelled
»
CHADEMA WATIKISWA MIOYO NA RASIMU YA KATIBA MPYA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment