Jana asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la
kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa
kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka
wa serikali.
Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu
aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote
wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na
wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni
lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa
Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.
Home
»
»Unlabelled
»
SUGU AISHINDA SERIKALI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment