Msanii nyota
toka kiwanda cha muvi za kibongo nchini Maulidi Mfaume maarufu kwa jina
la Gado Balotel sasa amekumbwa na balaa la aina yake baada ya kuvunjika
miguu yote miwili pamoja na nyonga kuteguka baada ya kudondoka toka
ghorofa ya nne alipokuwa akiigiza filamu ya msanii mwingine aitwae Baga.
Baada
Xdeejayz na kituo cha luninga cha DTV kupata taarifa hizo lilipiga hatua
ndefu hadi mahala anapojiuguzia msanii huyo ambako ni nyumbani kwa
msanii Wilson Fike maeneo ya Home Alone Vijana Kinondoni na kuonana uso
kwa uso na msanii huyo aneishi kwenye maumivu makali.
Akiongea na
mwandishi wetu nyumbani hapo Balotel alisema alikutwa na balaa hiyo wiki
mbili zilizopita akiwa Location ndani ya hotel ya Con Way iliyopo
Magomen Kagerana wasanii wenzake kama Hemed, Baga, Manaiki Sanga na wengineo wakati wakiigiza.
Balotel
aliendelea kusema kuwa wakati shughuri za kuigiza ziliendelea na kuna
sini moja iliyokuwa inahitajika kuigizwa kwa mfano ikimtaka mtu aigize
kama anataka kujirusha kwenye ghorofa lakini asiruke ili kameramankuchukua picha achukue shoti hiyo kisha mtu huyo aende chini kisha achukuliwe shoti nyingine ya kujifanya ametua chini.
Msanii huyo
aliendelea kusema kuwa nafasi hiyo ilibidi aigize msanii mwenye filamu
Baga lakini kutokana na uwoga wa msanii huyo alikuwa akijishauri namna
ya kuigiza kuruka ghorofani ndipo Ballotel akamtoa pembeni na kumuonesha
namna ya kuruka kama Jet Lee huku akimwambie mwenzake hiyo ilikuwa kazi
ndogo sana.
Msanii huyo
aliendelea kusema kuwa baada ya hapo alijikuta ameruka toka ghorofa ya
nne, lakini aliendelea kusema“ Wakati nikiwa bado sijashuka chini njiani
nilianza kuhisi harufu ya kifo kwani tayari nimuona Israel mtoa roho akinipungia mkono na hatimae nilitua chinikwa kufikia miguu” AlisemaBallotel
Hata hivyo
kijana huyo aliongeza kusema kuwa mala baada ya kutua nchini alihisi
moto unawake miguuni mwake huku harufu ya damu ikimtoka puani na mdomoni
na baada ya kujiangalia aliona visigino vyake vikiwa vimepasuka vyote
huku tumboni kukiwa na maumivu makali sana kumbe wakati huo nyonga ilikuwa imeachia huku miguu yake ikiwa imesogea tumboni.
Gado alisema
baada ya tukio hilo wasanii wenzake walimchukua na kukmimbiza Hospital
ya Mwananyamala mbapo dakika chache baadae walimkimbiza Muhimbili kwa
matibabu zaidi.Msanii huyo ambae ametamba sana kwenye filamu kama Going
Bongo,Msitu wa Hifadhi,Tumbo Joto na Escap ambayo alikuwa akiigiza siku
ya tukio lililomkuta.
Aidha msanii
huyo aliendelea kusema kwa sasa anaishi kwenye mateso makali huku
wasanii wenzake wakishindwa kumpa ushirikiana “Hapa nilipo nalelewa na
Fike Wilsoni ndiye anaenibeba kwenda chooni na kunirudisha kwa kweli
hali yangu sio nzuri nahitaji msaada wa wasanii wenzengu, Wako wanaokuja
kunirushia chochote kama
Kalapina,Young
Killer na madaktari wanasema huenda wakanishauri kwenda India ili
wakazirekebishe nyonga zangu” Alisema Gado na kuongeza kuwa anawaomba
wasanii wenzake wasamalia wema kumsaidia kwani hali yake ni mbaya na
huenda kwa mujibu wa madakatari wake akahitajika kupelekwa India ili
kukinusuru kiuno chake la sivyo hatozaa tena kwa vile nyonga
vimeshafyatuka
0 comments :
Post a Comment