TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Singida KIds
Moja ya story kubwa kuripotiwa na kituo cha ITV jioni ya jana ni ishu ya watoto watatu wa kiume kukutwa wakiwa wamejificha kwenye chasis ya basi.
Watoto hao wamekutwa Singida ambapo tayari walikuwa wamesafiri kutoka Kahama na walikuwa wakielekea Arusha.
Watoto hao wamesema walitolewa na mtu mmoja Arusha kwenda Kahama akawaambia kuna kazi, walipofika Kahama akawatelekeza, baadae wakaamua kurudi kwa njia hiyo ya kujificha kwenye chasis ya basi.
Kamanda wa Polisi Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema watoto hao walikutwa wakati wakaguzi wa mabasi walipokuwa wakikagua basi hilo la Mgamba Express ambapo mpaka wanafika hapo basi lilikuwa limesafiri kwa zaidi ya Kilometa 360.

0 comments :

 
Top